Pages

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Afanya Ziara Jeshi la Zimamoto

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga (wa pili kulia) akiwasili Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji yaliopo Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kwa ziara ya kikazi. Wa kwanza kulia ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Pius Nyambacha akimuongoza mara baada ya kumpokea.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Pius Nyambacha akimuonesha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga (hayupo pichani) kifaa maalumu kinachofungwa kwenye chumba kutambua tukio la moto kabla ya kuleta madhara makubwa na hupiga king'ora mara baada ya kuhisi tukio hilo. Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linataka majengo yote yafungwe kifaa hicho ili kukabiliana na madhara ya moto.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Pius Nyambacha (kulia) akitoa taarifa fupi ya utendaji kazi wa jeshi hilo pamoja na mafanikio kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga alipotembelea makao makuu ya jeshi hilo leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga (kushoto) akishauri jambo baada ya kupokea taarifa fupi ya utendaji kazi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika ziara yake aliyoifanya ambapo pia alitembelea kituo kikuu cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kilichopo Ilala Dar es Salaam kuangalia vifaa na shughuli za jeshi hilo. Kulia ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Pius Nyambacha.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga (kushoto) akipokea nyaraka kadhaa pamoja na taarifa fupi ya utendaji kazi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji toka kwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Pius Nyambacha katika ziara yake.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga (kushoto) akisalimiana na baadhi ya maofisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika ziara yake katika kituo kikuu cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kilichopo Ilala Dar es Salaam kuangalia vifaa na shughuli za jeshi hilo. 
Kituo cha kupokea taarifa za majanga ya moto cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kilichopo Ilala Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga (kushoto) akiwa katika Kituo Kikuu cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kilichopo Ilala Dar es Salaam. Kulia ni Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto Jesuald Ikonko akimuongoza.
Hapa akipata maelezo toka kwa mafundi wa karakana kuu ya Jeshi la Zimamoto Ilala Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga akipata maelezo ya namna vifaa mbalimbali vinavyotumiwa na jeshi hilo vinavyofanya kazi kwa baadhi ya vitengo vya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga (kushoto) akipata maelezo ya namna vifaa mbalimbali vinavyotumiwa na jeshi hilo vinavyofanya kazi kwa baadhi ya vitengo vya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya ziara yake katika ofisi za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)