Pages

WAZIRI UMMY MWALIMU ATEMBELEA MNADA WA NYAMA CHOMA DODOMA

IMG-20160123-WA0051
Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na wafanyabiashara wa eneo la Msalato lililopo mkoani Dodoma sehemu ambayo inatumika kufanyia mnada wa nyama choma ikiwa ni moja ya ziara zake kufatilia hali ya ugonjwa wa kipindupindu katika maeneo mbalimbali ya nchi, akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya hiyo, Dkt. Jasmine Tiisekwa (mwenye skafu shingoni) pamoja na Afisa Afya Mkuu wa Manispaa ya Dodoma Bw. Alek Barakena (mwenye suti nyeusi).
Na Rabi Hume, Modewjiblog
Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu ametembelea eneo la Msalato lililopo mkoani Dodoma sehemu ambayo inatumika kufanyia mnada wa nyama choma ikiwa ni moja ya ziara zake kufatilia hali ya ugonjwa wa kipindupindu katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Baada ya kutembelea mnada huo, Mhe. Ummy aliwataka wananchi wa eneo hilo kutambua kuwa bado ugonjwa wa kipindupindu upo na unaendelea kusambaa maeneo mbalimbali ya nchi hivyo ni wajibu wao kama wananchi kuweka mazingira yao katika hali ya usafi ili kutokomeza uonjwa huo.

Aidha ili kuzidi kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu, Waziri Ummy ameagiza kuendelea kutekelezwa kwa agizo la Mkuu wa Wilaya hiyo, Dkt. Jasmine Tiisekwa ambaye aliagiza kusimamishwa kwa shughuli za kuuza nyama nyoma katika eneo hilo la Msalato mpaka uongozi wa wilaya hiyo utakapojiridhisha kuwa ugonjwa wa kipindupindu umetoweka mkoani Dodoma.

“Kipindupindu kimesambaa sehemu nyingi nchini ikiwepo hapa Dodoma na hivyo naagiza katazo la Mkuu wa Wilaya, Dkt Jasmine Tiisekwa liendelee kuwepo hadi ugonjwa wa kipindupindu uishe Dodoma na niwajibu wa kila mwananchi kuhakikisha kipindupindu kinakwisha,” alisema Waziri Mhe. Ummy.

Pamoja na hayo pia Waziri huyo wa Afya ameutaka uongozi wa Manispaa ya Dodoma kufanya kikao cha pamoja na wafanyabiashara hao wa nyama choma ili kuona ni jinsi gani wanaweza kuendelea na biashara zao huku wakizingatia kanuni za usafi wa afya na mazingira bila kusababisha kuzidi kusambaa kwa kipindupindu.
IMG-20160123-WA0050
Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akifafanua jambo kwa wafanyabiashara wa eneo hilo.
IMG-20160123-WA0045
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akitoa maagizo ya wafanyabiashara hao kusitisha shughuli zao mara moja katika eneo hilo la Msalato mpaka uongozi wa wilaya hiyo utakapojiridhisha kuwa ugonjwa wa kipindupindu umetoweka mkoani Dodoma.
IMG-20160123-WA0043

IMG-20160123-WA0044
Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (wa pili kushoto), Mkuu wa Wilaya hiyo, Dkt. Jasmine Tiisekwa (wa tatu kulia) na Afisa Afya Mkuu wa Manispaa ya Dodoma Bw. Alek Barakena (kushoto) wakisikiliza hoja kutoka kwa mmoja wa wafanyabiashara wa eneo hilo (hayupo pichani).
IMG-20160123-WA0046
Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akisikiliza hoja kutoka kwa mmoja wa wafanyabiashara wa eneo la Msalato lililopo mkoani Dodoma sehemu ambayo inatumika kufanyia mnada wa nyama choma ambaye jina lake halikupatikana alipofanya ziara ya katika eneo hilo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)