Pages

Wafanyakazi wa TBL Mwanza wapigwa msasa wa elimu ya jinsia

 
 Mkaguzi Msaidizi wa jeshi la Polisi wa Dawati la Jinsia wilaya ya Kinondoni Inspekta Prisca Komba akitoa mafunzo ya jinsia kwa wafanyakazi wa kiwanda cha TBL Mwanza .Mafunzo haya yanaendelea katika viwanda vyote vilivyopo chini ya TBL Group nchini
 Wafanyakazi wa TBL Mwanza wakimsikiliza Bi.Enid Muro,mmoja wa watoa mada katika semina hiyo.
Meneja Uhusiano wa kampuni ya kampuni ya TBL Group,Editha Mushi akiongea na wafanyakazi wa kiwanda cha bia cha Mwanza wakati wa semina ya masuala ya jinsia iliyofanyika mkoani humo jana.Semina kuhusiana na masuala ya jinsia  kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo imefanyika pia kwenye viwanda vyake tanzu nchini kote na kuendeshwa na Mkaguzi Msaidizi wa jeshi la Polisi wa Dawati la Jinsia wilaya ya Kinondoni Inspekta Prisca Komba

Elimu ya masuala la Jinsia ambayo imekuwa ikitolewa  kwa wafanyakazi wa makampuni tanzu ya TBL group kwa wiki tatu mfululizo jana yaliwafikia wafanyakazi wa kampuni hiyo wa kiwanda cha kutengeneza bia cha Mwanza.
 
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Mwanza ambao walipata fursa ya kuhudhuria mafunzo hayo ambayo yameendeshwa na Mkaguzi Msaidizi wa jeshi la Polisi wa Dawati la Jinsia wilaya ya Kinondoni Inspekta Prisca Komba wamesema yamewawezesha kuelewa masuala mbalimbali yanayohusiana na jinsia.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)