Pages

Amana Fc yaichabanga Dar Community bank FC magoli 8-1!

Kikosi cha Amana FC ikiwa tayari kwa mchezo hapo juzi.

Timu ya mpira wa miguu ya Amana Bank FC juzi iliichabanga timu ya Dar Community Bank mabao 8-1 katika mchezo wa mashindano ya mabenki yanayoendelea katika uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo ambao Amana Fc iliutawala kwa vipindi vyote viwili, ikiongozwa na nahodha wao Muhsin Mohmed aliyefunga magoli matatu, huku kiungo mchezeshaji wa timu hiyo machachari  Ally Khamisi akiifungia mabao matatu pia kabla Anthony Mahimbali na Ally Abdul wakihitimisha karamu hiyo ya magoli. 

Awali Amana Fc ilicheza na Access Bank Fc katika mcheko mkali na wa kusismua ambapo timu hizo zilitoka sare kwa kufungana mabao mawili kwa mawili, matokeo hayo yameifanya Amana Fc kuongoza msimamo wa ligi  hiyo ya mabenki ambayo inashiriki kwa mara ya kwanza mwaka huu ikiwa na pointi 7 na magoli 13. Amana Fc ipo katika kundi B ambalo lina timu za Mkombozi Fc, Access bank na wenyewe Amana Fc.

Amana Fc imejikuta ikiingia robo fainali ya mashindano hayo baada ya kupewa ushindi wa pointi 3 na magoli matatu baada ya timu ya Mkombozi kutotokea uwanjani hivyo wakazawadiwa ushindi wa chee. Akiongea na mtandao huu meneja masoko wa benki hiyo Juma Msabaha Jr amesema vijana wao wapo vizuri na wana matarajio mazuri kushinda mechi yao ya robo fainali ambayo itachezwa baadae wiki hii katika uwanja wa Karume jijini Dar.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)