Mkaguzi Msaidizi wa jeshi la
Polisi wa Dawati la Jinsia wilaya ya Kinondoni Inspekta Prisca Komba akitoa
mafunzo ya jinsia kwa wafanyakazi wa kiwanda cha TBL Mbeya .Mafunzo haya
yanaendelea katika viwanda vyote vilivyopo chini ya TBL Group nchini
Afande Prisca akiwazungukia washiriki wakati wa semina
Baadhi wa wafanyakazi wa TBL Mbeya wakimsikiliza afande Prisca wakati huo huo wakipata chakula cha mchana.
5.Baadhi wa wafanyakazi wakiburudika na kupata maarifa baada ya saa za kazi wakati wa mafunzo hayo awamu ya jioni
Baadhi wa wafanyakazi wakiburudika na kupata maarifa baada ya saa za kazi wakati wa mafunzo hayo awamu ya jioni
Wafanyakazi wa kampuni ya TBL Group katika kiwanda cha Mbeya leo
wamepatiwa semina kuhusiana na masuala
ya jinsia na Mkaguzi Msaidizi wa jeshi la Polisi wa Dawati la Jinsia
wilaya ya Kinondoni Inspekta Prisca Komba.
Katika semina hiyo wafanyakazi waliweza kujua masuala mbalimbali
yanayohusiana na masuala ya kijinsia ambapo pia walipata fursa ya kuuliza
sheria na masuala ya jinsia kutoka kwa mkufunzi huyo kutoka Jeshi la Polisi.
Baadhi ya wafanyakazi walioshiriki mafunzo hayo walisema kuwa yameweza
kuwafumbua macho kujua masuala mbalimbali yatakayowasaidia katika maisha yao ya
kila siku wanapokuwa sehemu za kazi na katika maisha ya kawaida na familia zao
wanapokuwa wameishatoka kazini.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)