Pages

Uzinduzi wa Jumuiya ya Veterani wa Umoja wa Vijana Zanzibar Young Pioneers.

Maveterani wa Umoja wa Vijana wa Young Pioneers wakipiga makofi wakati wa kuingia mgeni rasmin Mhe Waziri wa Fedha Omar Yussuf Mzee kwa ajili ya uzinduzi wa Jumuiya hiyo kuendeleza Vijana Zanzibar.
Maveterani wa Umoja wa Vijana wa Young Pioneers wakipiga makofi wakati wa kuingia mgeni rasmin Mhe Waziri wa Fedha Omar Yussuf Mzee kwa ajili ya uzinduzi wa Jumuiya hiyo kuendeleza Vijana Zanzibar.
Ustadh akisoma Quran kabla ya Uzinduzi huo wa Jumuiya ya Veterani wa Umoha wa Vijana wa Young Pioneers uliofanyika katika ukumbi wa ZSSF kiwanja cha Watoto Kariakoo Zanzibar.
Maveterani wa Young Poineers wa Umoja wa Vijna wakimsikiliza msoma quran wakati wa uzinduzi huo.
Katibu wa Veterani wa Young Pioneers Said Shaban akitowa maelezo ya Jumuiya hiyo ya Veterani wa Umoja wa Vijana wa Young Pioneers wakati wa Uzinduzi wake uliofanyika katika Ukumbi ZSSF Kiwanja cha Watoto Kariakoo Zanzibar. 
Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Jumuiya ya Veterani wa Young Pioneers, Mhe. Khadija Hassan Aboud akizungumza wakati wa hafla hiyo ya Uzinduzi wa Jumuiya hiyo. 
 Katibu Mkuu Wizara ya Ustawi wa Jamii Maendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto Mhe Asha Ali Abdalla akizungumza wakati wa hafla hiyo ya Uzinduzi wa Jumuiya ya Veterani ya Umoja wa Vijana wa Young Pioneers, katika Ukumbi wa ZSSF Kiwanja cha Watoto Kariakoo Zanzibar.
Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf Mzee akiwahutubia Veterani wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Young Pioneers wakati wa Uzinduzi wa Jumuiya hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa ZSSFKiwanja cha Watoto Kariakoo Zanzibar. na kutangaza Fedha zilizopatika katika harambee aliyoiazisha kwa ajili ya kukuza Mfuko wa Jumuiya hiyo Jumla ya Shilingi Milioni 9,724,000/= zimepatika ikiwa Fedha Taslimu Shs 3.874,500 na Ahadi Shs.5,850,000/=
Wanachama wa Jumuiya ya Veterani wa Young Pioneers wakimsikiliza mgeni rasmin akiwahutubia wakati wa Uzinduzi wa Jumuiya yao.
Veterani wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Young Pioneers wakimsikiliza mgeni rasmin wakati akiwahutubia na kuwazindulia Jumuiya yao.
Wazee Maveterani wa Young Pioneers wakiwa meza kuu wakimsikiliza Mgeni rasmin Mhe Omar Yussuf Mzee akiwahutubia wakati wa uzinduzi huo wa Jumuiya hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa ZSSF Kiwanja cha Watoto Kariakoo Zanzibar. 
Maveterani wakichangia katika harambee hiyo ya Uzinduzi wa Jumuiya hiyo
Maveterani wakichangia katika harambee hiyo ya Uzinduzi wa Jumuiya hiyo
Veterani wa Umoja wa Vijana aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Tanzania Mhe Sukwa Said Sukwa akichangia katika harambee hiyo, ya Uzinduzi wa Jumuiya hiyo.
Veterani wa Young Pioneers Mhe. Aboud Talib Aboud akichangia wakati wa uzinduzi wa Jumuiya hiyo. baada ya kuitishwa upato wa maridadi na kupatikana shilingi milioni 9,724,000/= papo kwa papo wakati wa harambe hiyo ya Veterani wa Young Pioneers.
Veterani wa Young Pioneers Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe Abdalla Mwinyi Khamis akichangia wakati wa uzinduzi wa Jumuiya hiyo. 
Mjumbe wa Kamati ya Jumuiya ya Veterani wa Umoja wa Vijana wa Young Pioneers Meja Generali Mstaaf Hassan Vuai Chema, akitowa neno la shukrani kwa Mgeni rasmin Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf Mzee baada ya kuwazinduliwa Jumuiya yao katika ukumbi wa ZSSF Kiwanja cha Watoto Kariakoo Zanzibar. 
Veterani wa Young Pioneers Makame Haji Makame (Cairo) akihamasisha kwa kuimbi wimba za Vijana za wakati huo wa kuhamasisha vijana katika kujenga taifa wakati wa uzinduzi wa Jumuiya hiyo katika ukumbi wa uwanja wa watoto kariakoo Zanzibar, kabla ya kuaza kwa kongamano la Jumuiya hiyo
 Mwenyekiti wa Kongamano hilo la Veterani wa Young Pioneers Mhe Aboud Talib Aboud akiongoza kongamano hilo likizungumzia kumkomboa Kijana.katika kujiajiri na kujiengezea kipato.na kuwa na maadili mazuri.  
MTOA Mada katika Kongamano hilo la Uzinduzi wa Jumuiya ya Maveterani ya Young Pioneers Association Ndg Ali Khamis akitowa Mada kuhusu Wajibu kwa Kijana, kwa wajumbe wa mkutano huo wa uzinduzi uliofanyika ukumbi wa kiwanja cha watoto kariakoo Zanzibar
Veterani wa Young Pioneers wakimsikiliza Mtoa Mada juu ya Maendeleo ya Vijana katika kujikomboa Kiuchumi.
Veterani wa Young Pioneers wakiwa katika ukumbi wa mkutano wakato wa Kongamano.
Mgeni Rasmin Mhe Omar Yussuf Mzee akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Jumuiya ya Veterani wa Umoja wa Vijana  Young Pioneers wa wakati huo wa Umoja wa Vijana Zanzibar. Baada ya Kuizindua Jumuiya hiyo. Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot. Zanzinews.com.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)