Imekuwa
ni kawaida kwa watumiaji wengi kununua matairi ya magari yao bila
kujali viwango vya matairi hayo ili mradi tu mtu kanunua. Kwenye Kununua
matairi kuna vigezo vingi sana vinavyopelekea kuwa tairi kuwa sahihi
katika mahitaji yako.
Mfano
wa vitu hivyo ni Ukubwa wa tairi (size ya tairi), upana, na urefu wa
tairi na uwezo wa mwisho wa spidi gari inapokimbia lakini wengi wamekuwa
wakiangalia vitu vichache kama Upana, na Urefu tu bila kuangalia spidi
inayotakiwa kukimbia katika matairi hayo kwa kingereza uitwa Tyre Speed
rating ambapo matairi yote huwa yana ukomo wa spidi endapo gari
inatembea.
Leo
sasa tutakuangalizia jinsi ya kuweza kutambua spidi ya mwisho
unayotakiwa kukimbia kutokana na matairi ya gari yako. Jinsi ya kutambua
unachotakiwa kufanya ni kuangalia kwenye tairi yako kuna sehemu
imeandikwa kwa mfano huu "255/65/R16 91W" Maana ya tarakimu hizo ni 255
ni upana wa tairi, 65 ni urefu wa tairi kutoka kwenye rim, R16 ni saizi
ya rim na hiyo 91W ndio tairi speed rating yenyewe. Kwa mfano huo juu
gari lenye tairi hilo spidi rating yake ni W ambayo unatakiwa kutembea
spidi ya mwisho ni 168 Miles/hour au 270Km/hour.
Na hii ndio chati ya Speed rating ya tairi zote unachotakiwa kuangalia ni Herufi
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)