Pages

Mwili wa marehemu Leticia Nyerere wawasili nchini, Kuagwa leo kabla ya kusafirishwa kuelekea Butiama kwa mazishi kesho

 Askari wa Bunge wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mara, Leticia Nyerere aliyefariki nchini Marekani alikokuwa akitibiwa mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam jana jioni. Mwili huo utaagwa leo nyumbani kwa Mwalimu Nyerere Msasani  kabla ya kusafirishwa kwenda Butihama mkoani Mara kwa mazishi yatakayofanyika kesho
 Mwili huo ukiingizwa kwenye gari maalumu katika uwanja huo.
 Ndugu jamaa na marafiki wakijadiliana jambo wakati wa kuupokea mwili huo.
 Ndugu, jamaa, marafiki na watoto wa marehemu wakisubiri kuupokea mwili wa mpendwa wao.
 Mume wa marehemu, Madaraka Nyerere akizungumza na wanahabari baada ya kuupokea mwili huo uwanjani hapo.
Mtoto wa marehemu (kulia), akifarijiwa na mmoja wa ndugu wakati wakienda kupanda gari kabla ya kuondoka uwanjani hapo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)