Pages

Mwigizaji wa Hollywood alikutana na El Chapo

 
 Sean Penn na El Chapo 

Maafisa wa serikali nchini Mexico wamesema walijiandaa kumkamata kinara wa uuzaji wa madawa ya kulevya Joaquin Guzman maarufu kama El Chapo baada ya kufanya mahojiano na mwigizaji wa Hollywood Sean Penn.

Inasemekana serikali ilikuwa ikifuatilia nyendo za bwana Penn baada ya kukutana kwa siri na kinara huyo wa madawa ya kulevya katika eneo lililojificha mwezi October mwaka jana.

Katika mahojiano na jarida la Rolling Stone, El Chapo Guzman alisema yeye ndiye baba wa biashara ya madawa ya kulevya duniani ambapo anasafirisha kwa ndege na meli za chini kwa chini mwa bahari.
Bwana Penn alisema alifanya mahojiano hayo kwa sababu Wamerekani ni sehemu ya watumiaji wakubwa wa madawa hayo yenye athari na vurugu za mauaji.

Wakati huo huo Mexico imesema inajiandaa kumsafirisha El Chapo Guzman nchini Marekani ili kwenda kuyakabili mashitaka yake lakini wanasheria wake wanasema watapambana kuzuia suala hilo.Chanzo BBC Swahili

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)