Wanafunzi
John Method (kushoto) na Edwin Luguku (wa pili kulia) kutoka Shule ya
Sekondari Mzumbe mkoani Morogoro wakipokea hati zao za ufadhili kutoka
kwa Karimjee na Ofisa Ubalozi wa Ireland nchini, Bi. Carlo. Wanafunzi
hao waliibuka washindi wa jumla katika maonesho ya Sayansi kwa Shule za
Sekondari mwaka 2015 yanayoandaliwa na taasisi ya Young Scientists
Tanzania (YST). (Picha zote na Daniel Mbega wa www.brotherdanny.com).
Ofisa
Ubalozi wa Ireland nchini, Bi. Carlo, akizungumza na Edwin Luguku na
John Method kutoka Shule ya Sekondari Mzumbe, Morogoro ambao waliibuka
washindi wa jumla katika maonesho ya Sayansi kwa Shule za Sekondari
mwaka 2015 yanayoandaliwa na taasisi ya Young Scientists Tanzania (YST).
Wanafunzi hao wanaondoka leo hii kwenda Dublin, Ireland kwa maonesho ya
sayansi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa taasisi ya Young Scientists Tanzania (YST), Dk. Gozibert
Kamugisha, akizungumza wakati wa kukabidhiwa kwa scholarship kwa
wanafunzi Edwin Luguku na John Thomas wa Shule ya Sekondari Mzumbe ambao
walikuwa washindi wa jumla katika maonesho ya sayansi 2015. Wanafunzi
hao walipewa scholarship hizo la taasisi ya Karimjee Jivanjee Foundation
ya jijini Dar es Salaam.
Meneja
wa taasisi ya Karimjee Jivanjee Foundation, Devota Rubama, akizungumza
kabla ya kukabidhi hati za ufadhili kwa wanafunzi Edwin Luguku na John
Thomas wa Shule ya Sekondari Mzumbe, Morogoro walioshinda katika
maonesho ya sayansi 2015.
Mzee Karimjee, Mwenyekiti wa Taasisi ya Karimjee Jivanjee Foundation.
Toyota Tanzania Limited nao waliwazawadia vijana hao kwa ushindi walioupata.
Na Daniel Mbega wa brotherdanny.com
TAASISI
ya Karimjee Jivanjee Foundation ya jijini Dar es Salaam leo hii
imekabidhi scholarship kwa wanafunzi wawili wa Shule ya Sekondari
Mzumbe, Morogoro, ambao waliibuka washindi wa jumla katika Maonesho ya
Tano ya Sayansi ya YST kwa Shule za Sekondari Tanzania Agosti 2015.
Wanafunzi
hao, Edwin Luguku na John Method, ambao leo hii wanakwenda jijini
Dublin, Ireland kuhudhuria Maonesho ya 53 ya Sayansi, waliibuka washindi
kutokana na utafiti wao wa sayansi usemao “Madhara ya Matumizi ya
Mifuko ya Plastiki Tanzania na Namna ya Kupunguza Matumizi hayo” (The
Effects of Using Plastic Bags in Tanzania and How to Reduce the Same).
Kutokana
na udhamini huo, wanafunzi hao wawili ambao wanatarajia kumaliza kidato
cha sita mwaka huu, watasomeshwa na taasisi hiyo chuo kikuu huku
wakilipiwa ada pamoja na gharama nyingine zote kwa miaka yote
watakayokuwa wanachukua shahada zao.
Itakumbukwa
kwamba, Taasisi ya Karimjee Jivanjee mbali ya kutoa scholarship kwa
wanafunzi hao, pia ilitoa ufadhili kwa shahada ya kwanza chuo kikuu kwa
wanafunzi Petro Samson Ndegeleki na Juma Joshua Wiliam kutoka Nassa
Sekondari ya Simiyu ambao utafiti wao ulihusu ‘How Different Natural
Fertilizers Affect the Growth Of Maize’.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)