JK ahani msiba wa aliyekuwa mkurugenzi wa TAA, Mhandishi Suleman Said Suleiman - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

JK ahani msiba wa aliyekuwa mkurugenzi wa TAA, Mhandishi Suleman Said Suleiman

 RAIS mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisjo Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na watoto watatu wa marehemu Mhandisi Suleiman Said Suleiman, aliyekuwa mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Nchini, TAA, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Upanga jijini Dar es Salaam, leo Januari 19, 2016 kutoa mkono wa pole. Marehemu Suleiman alifariki Jumatatu Januari 18, 2016 wakati akifanya mazoezi ya kuogelea kwenye bahari ya hindi na tayari amezikwa. (Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)

RAIS mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, leo Januari 19, 2016 amehani msiba wa aliyekuwa Mkurugezi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini, marehemu Mhandisi Suleiman Said Suleiman.


Dkt. Kikwete aliwasili nyumbani kwa marehemu Upanga jijini Dar es Salaam, akifuatana na mkewe Mama Salma Kikwete majira ya saa 10;30, akitokea kijijini kake Msoga mkoani Pwani.

Baada ya kiwasili, nyumbani kwa marehemu Rais mstaafu alipokewa na mdogo wa marehemu, Mhandisi, Nasiri Said Suleiman, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Bw.  Laurent Mwigune, Mkurugenzi wa Sheria na Mawasiliano ya umma, Bw. Ramadhan Maleta, maafisa wa TAA, na wanafamilia wengine na kwenda moja kwa moja kuweka saini kitabu cha maombolezo. Baada ya kufanya mazungumzo kwa muda, Watoto wawili wa marehemu ambao wanasoma nje ya nchi nao waliwasili na kupata fursa ya kusalimiana na Rais mstaafu, Dkt. Kikwete.

Watoto hao ni pamoja na motto mkubwa wa marehemu, Mohammed Said Suleiman, na mdogo wake Said Suleiman Said. Baadaye Rais alikwenda kusaliamiana na mama mzazi wa marehemu, mke wa marehemu na
wafiwa wengine na kasha yeye an msafara wake kuondoka majira ya saa 11 jioni. Mhandisi Suleiman Said Suleima, alifariki dunia Januari 18, 2016 majira ya asubuhi wakati akifanya mazoezi ya kuogelea kwenye bahari ya hindi katikati ya Magogoni na Kigamboni na kuzikwa jioni ya siku hiyo hiyo.
Marehemu ameacha mjane na watoto watatu, Mohammed, Said na Hosam.
 Akisaini kitabu cha maombolezo
 JK akisalimiana na Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano wa TAA, Bw. Ramadhan Maleta
 JK akimpa pole mtoto wa mwishi wa marehemu, Hosam Suleiman Said Suleiman
 JK akimpa pole mtoto mkubwa wa marehemu, Moahmmed Suleiman Said Suleiman
 JK akimsikiliza Mkurugenzi wa  Rasilimali Watu Utawala wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini, TAA, Bw.Laurent Mwigune
 JK akisalimiana na mdogo wa marehemu, Mhandisi Nasiri Said Suleiman
 JK akimpa pole mama wa marehemu
 Mama Salma Kikwete, akitoka nyumbani kwa marehemu Mhandisi Suleiman Said, baada ya kuhani msiba wake Januari 19, 2016
 JK akisalimiana na Mkurugenzi wa Kazi Maalum wa TAA,  Mhandis Thomas Junior Haule
 JK akisalimiana na Meneja Rasilimali Watu na Utawala, Bw. Mohamed R.Ally

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages