Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (kushoto) akishauriana na
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Abbas Kandoro (kulia) namna ya kutatua changamoto ya
usafirishaji mizingo katika forodha ya Tunduma.
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Kijaji (kushoto) akiongea na watendaji wa
TRA Mbeya alipowatembelea ofisini kwao kujua matarajio yao pamoja na changamoto
wanazokumbana nazo katika utendaji kazi. Kulia kwake ni Bw. Lucas Mnabi Kaimu
Meneja TRA Mbeya.
Mkuu
wa Hazina Ndogo Mbeya Bw. Siwale (aliyesimama)
akitoa ufafanuzi kwa Mhe. Dkt. Kijaji namna wanavyowahudumia wastaafu. Na
kushoto kwake ni wafanyakazi wa Hazina Ndogo Mbeya.
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Kijaji (katikati) akiandika dondoo za ujio
wake katika ofisi za Mhakikimali Mkoa wa Mbeya. Aliyesimama ni Katibu wa Naibu
Waziri Fedha na Mipango na Mchumi Bw. Moses Dulle akitoa utangulizi kabla ya
kuanza majadiliano. Kulia ni Mhakikimali Mkoa wa Mbeya Bw.
Simon Njoka na pembeni yake ni Mkuu wa Hazina Ndogo Mbeya Bw. Siwale. Picha
na Eva Valerian Afisa Mawasiliano, Kitengo
cha Mawasiliano - Wizara ya Fedha na Mipango
Akizungumza na Meneja
wa Oparesheni ambaye ni Kaimu Mkurugenzi
wa Benki Kuu Mbeya Bw. Ibrahim Malongo, Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt.
Ashatu Kijaji alisema kumekuwa na ubadilishanaji fedha isio halali unaofanyika kiholela
hapa Tunduma unaopelekea Serikali kukosa mapato.
Mhe. Dkt. Kijaji
alifanya ziara hiyo eneo la tukio huko Tunduma na kujionea namna vijana hao wanavyofanya
biashara hiyo bila wasiwasi wowote huku wakiwa wameshika fedha nyingi sana
mikononi.
“Nakupa siku tatu,
nataka unijulishe hali hii (black market) iko vipi kwa sasa, mikakati gani
ambayo mmeipanga kwa sasa, nini kimefanyika na hatua gani zimechukuliwa ili
kuiwezesha Serikali kupata mapato.” Mhe. Dkt. Kijaji alimwambia na kumsisitiza
Meneja wa Oparesheni ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Benki Kuu Mbeya Bw. Ibrahimu
Malongo.
Katika ziara hiyo
Mhe. Dkt. Kijaji aliutaka uongozi wa
Benki Kuu Mbeya kufuatilia wakopeshaji wanaojiendesha kinyume na taratibu kwa
kuwakopesha wananchi tena kwa riba kubwa bila kulipa kodi.
Hivyo amemuagiza
Kaimu Mkurugenzi Bw. Malongo na amempa siku saba kulifuatilia suala hilo kwa
karibu, kujua wakopeshaji hao wako wangapi, na wana mikakati gani ya kuiweka
kihalali biashara hiyo ili wakopeshaji hao waweze kusimamiwa kwa sheria kanuni
na taratibu bila kumuumiza mwananchi na waweze kulipa kodi.
Mhe. Dkt. Kijaji alishauri
Taasisi zilizorasmi ambazo zinakopesha kupunguza masharti yasiyo na tija ili
kuwasaidia wananchi waweze kukopesheka na waweze kulipa ili maisha yao yaweze
kuendelea.
Katika ziara yake
Mhe. Dkt. Kijaji alipata fursa ya kuonana na uongozi wa TRA, Mkuu wa Mkoa wa
Mbeya Mhe. Abbas Kandoro, Hazina Ndogo na alipata fursa ya kuongea na Mkuu wa
Hazina Ndogo Bw. Siwale pamoja na Mhakikimali Mkoa wa Mbeya Bw. Simon Njoka.
Aliwasisitiza kufanya kazi kwa bidii na kuwataka wawe jicho la Serikali ndani
ya Mbeya kwa kuangalia hasa utendaji kazi na kusimamia maadili ya kazi.
Imetolewa
na Kitengo cha Mawasiliano
Wizara
ya Fedha
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)