BALOZI WA NORWAY NCHINI TANZANIA ATEMBELEA KITUO CHA KUZALISHA UMEME CHA KIKULETWA WILAYA YA HAI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

BALOZI WA NORWAY NCHINI TANZANIA ATEMBELEA KITUO CHA KUZALISHA UMEME CHA KIKULETWA WILAYA YA HAI

Balozi wa Norway nchini Tanzania ,Hanne -Marie Kaarstad akiweka saini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye Kituo cha kuzalisha umeme na kutoa mafunzo cha Kikuletwa ambacho nchi yake imetoa dala za Marekani milioni 5 kwaajili kukifufua kwaajili matumizi ya Chuo cha Ufundi Arusha(ATC)
Kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro,Anthony Mtaka,Balozi wa Norway nchini Tanzania ,Hanne -Marie Kaarstad na Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC),Dk Richard Masika wakikagua vyanzo vya maji eneo la Chemka vitakavyotukika kuzalisha umeme na kutoa mafunzo kwa wanafunzi wa fani ya Uandisi Umeme wa Chuo hicho.

Mhandisi wa Umeme katika Chuo cha Ufundi Arusha,Merchior Urbanus(kushoto)akimwelekeza jambo Balozi wa Norway wakati akitembelea eneo la Kikuletwa.
Balozi wa Norway nchini Tanzania ,Hanne -Marie Kaarstad akifurahia madhari ya Kituo cha Kikuletwa, amehaidi kuendelea kusaidia sekta ya nishati hapa nchini.
Moja ya mitambo zamani iliyopo kwenye kituo cha Kikuletwa iliyowekwa na Mmisionari wa Kijerumani mwaka 1935 na baadaye kukabidhiwa kwa shirika la umeme nchini Tanesco kisha Chuo cha Ufundi Arusha baada ya kutotumika kwa muda mrefu.
Moja ya chanzo cha maji ambacho pia hutumika kama sehemu ya utalii kutokana na maji yake kuwa ya vuguvugu muda wote.


Balozi wa Norway nchini Tanzania ,Hanne -Marie Kaarstad(wa tatu kutoka kulia)Mkuu wa Chuo hicho,Dk Richard Masika wakiwa katika picha ya pamoja na Manaibu Wakuu wa Chuo hicho na maafisa wa Ubalozi wa Norway nchini katika picha ya pamoja leo. Imeandaliwa na www.rweyemamuinfo.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages