Pages

BALOZI MASILINGI AHANI MSIBA WA LETICIA NYERERE LANHAM, MARYLAND

 Wapili toka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi akitoa pole kwa Madaraka Nyerere ( wakwanza kushoto) mume wa marehemu Leticia Nyerere nyumbani Lanham, Maryland nchini Marekani siku ya Jumatatu January 11, 2016. Wengine kwenye picha ni Emmanuel Muganda na Mwenyekiti wa CHADEMA DMV Kalley Pandukizi (kulia). PICHA NA VIJIMAMBO/KWANZA PRODUCTION
 Kutoka kushoto ni Zuberi, Afisa Ubalozi Swele na Mwambata wa Jeshi Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na Canada Colonel Adolph Mutta.
Wanne toka kushoto ni Mke wa Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Marystella Masilingi akiongea jambo na Swahiba Mdeme Mkuu wa Utawala na Fedha Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani (wapili toka kulia). Kulia ni Mrs Muganda wakijumuika na wafiwa katika kuwafariji katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.
Afisa Ubalozi Suleiman Saleh akiwa na Katibu Muenezi na Itikadi CCM DMV Bi. Salma Moshi  wakihani msiba wa marehemu Leticia Nyerere aliyeaga Dunia siku ya Jumapili January 10, 2016 katika hospitali ya Jumuiya ya Madakatari iliyopo Lanham, Maryland nchini Marekani.
NY Ebra (kulia) akitoa pole kwa Madaraka Nyerere mara tu alipofika yeye na Dkt Temba wakitokea New York.


No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)