Ofisa Mipango wa Kampuni ya TBL Group kutoka Dar es Salaam, Tumaini Moses akiwasili kwenye
Uwanja wa ndege wa Songwe mkoani Mbeya akiwa na Kombe la tuzo ya
Mwajiri bora 2015 ambayo kampuni hiyo
ilishinda hivi karibuni.Hafla yakupokea kombe ilifanyika mwishoni mwa wiki
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL wa Mbeya katika
picha ya pamoja wameshikilia kombe la ushindi.
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL wa Mwanza katika
picha ya pamoja wameshikilia kombe la ushindi
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Mwanza katika picha
ya pamoja wakati wa hafla ya kushangilia ushindi iliyofanyika mwishoni mwa wiki
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Dar es Salaam katika picha ya pamoja wameshikilia kombe la ushindi
Dar
es –Salaam Desemba 20,2015: Wafanyakazi wa kampuni ya Tanzania Breweries Limited Group
katika mikoa ya Dar es Salaam,Mwanza,Mbeya na Arusha wameshiriki kusherehekea
mafanikio ya kampuni yao kwa kuibuka
mshindi wa tuzo ya mwajiri bora
kwa mwaka 2015 ambayo ilitunukiwa hivi karibuni na Chama Cha Waajiri Tanzania
(ATE).
Ushindi huu umekuwa shirikishi kwa
wafanyakazi wote ambapo kombe la tuzo hiyo limetembezwa katika viwanda vya
kampuni vilivyopo katika mikoa mbalimbali ambapo wafanyakazi walilipokea na
kufanya hafla za kusherehekea ushindi huo.
Mkurugenzi wa Raslimali Watu wa TBL
Group David Magese alisema kuwa ushindi huu na mafanikio mengine ya kampuni hayahusu
uongozi pekee bali wafanyakazi wote wa kampuni “ushirikishwaji wa wafanyakazi wote katika mafanikio yetu ni
jambo ambalo tunalizingatia sana na ndio maana tumeamua kulizungusha kombe hili
la tuzo ya mwajiri bora kwao ili washerehekee ushindi huu kwa kuwa ni miongoni
mwa wadau wakubwa wa mafanikio haya”.Alisema.
Magese aliongeza kusema kuwa TBL Group
ambayo pia inashikilia tuzo ya Mlipa
Kodi bora nchini mbali na ushindi huu wa jumla mwaka huu pia ilishinda tuzo
zingine tofauti ambazo ni Uzingatiaji Kanuni Bora za Uongozi,Uongozi na
Utawala,Uzingatiaji wa Kanuni za Raslimali Watu ,Ubora na Uzalishaji,Kujari na
kuthamini walemavu na tuzo ya Taasisi Bora inayoongoza kwa Ukubwa.
“Mwaka jana kampuni ya TBL ilishinda
tuzo ya jumla katika kipengele cha Mahusiano mazuri na wafanyakazi ambayo
inadhihirisha kuwa kampuni imeweka mazingira bora ya kufanyia kazi na inawajali
wafanyakazi wake katika ngazi zote.Tuzo hiyo pia ilitambua kuwa TBL imejenga
mazingira bora na uongozi makini unaozingatia vigezo bora vya ajira na kujenga
mazingira mazuri ya kazi kwa waajiriwa wake”.
Alimalizia kwa kusema kuwa kampuni hiyo
inao wafanyakazi 2,100 nchini kote wakiwa wanafanya kazi za ufundi,Mauzo na
Usambazaji,na katika vitengo mbalimbali vya biashara na kati ya hao wapo wenye
ajira za kudumu na ajira za muda na kuongeza kuwa itaendelea kutoa motisha kwa
wafanyakazi,kujali afya zao na kuzingatia zaidi kanuni za usalama kazini pia
kuwaendeleza wafanyakazi wake kimafunzo ili kuongeza ufanisi zaidi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)