Pages

UNODC YAKABIDHI VIFAA VYA MAABARA JESHI LA MAGEREZA

Afisa Mipango wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC), Immaculata Nyoni akizungumza jambo kabla ya kukabidhi vifaa vya maabara kwa Jeshi la Magereza nchini.
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akizungumza jambo wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa vifaa vya maabara kwa Magereza Tanzania.
DSC_0126

Afisa Mipango wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC), Immaculata Nyoni pamoja na Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa wakikata utepe kuashiria kukabidhiwa vifaa vya maabara vilivyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC).

Afisa Mipango wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC), Immaculata Nyoni akitolea ufafanuzi vifaa vya maabara alivyokabodhi kwa Jeshi la Magereza ili kusaidia kuwapima wafungwa walioko magerezani.

Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa akitoa shukrani baada ya kupokea msaada kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC) lililowakilishwa na Immaculata Nyoni.


Hivi ndivyo vifaa vya maabara vilivyokabidhiwa kwa Jeshi la Magereza.


Picha ya pamoja.

Na Mwandishi wetu

Jeshi la Magereza Ukonga limepokea vifaa vya maabala kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC) ambavyo vitasaidia kutoa vipimo kwa wafungwa waliofungwa magerezani hii ikiwa ni jitihada za kupunguza matumizi ya dawa za kulevya katika magereza hapa nchini.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo Bi. Immaculata Nyoni ambaye ni Afisa Mipango wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC) alisema wametoa msaada huo baada ya kufanyika kwa tafiti hasa kwenye magereza hapa nchini na utafiti huo Magereza ilishirikiana na UNODC na kubaini changamoto wanazozipata wafungwa wakati wa kupimwa afya zao. Hivyo kama shirika limeamua kutoa msaada wa vifaa vya maabala ambavyo ni Hematology mbili(2), Urine Analyzer tatu (3) pamoja na Hemoglobin Mashine mbili(2) na vifaa hivi vimegharimu takribani shilingi milioni 10 za kitanzania.

Akitoa shukrani Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa kwa niaba ya Mkuu wa Magereza hapa nchini amesema anawashukuru UNODC kwa kuona matatizo yanayowakabili hasa kwenye hospitali za Magereza zinazohudumia wafungwa na kuamua kutoa msaada huo kwa jeshi hilo.

Pia alisisitizaushirikiano kati ya Jeshi la Magereza pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC) kuimarishwa ili kuweka ukaribu kwa kila jambo linalohusu afya ya wafungwa hasa kwa wale waliokuwa wanatumia madawa ya kulevya na wenye virusi vya UKIMWI.

Baada ya wauguzi kupokea msaada huo walisema sasa ni muda wa kazi tu kwani wamepata vifaa ambavyo vitaweza kuwahudumia wagonjwa kwa wakati kwani hapo mwanzo kulikuwa na uhaba wa vifaa vya maabara na kupelekea matibabu kutokuwa ya uhakika katika hospitali za Magereza zinazohudumia wafungwa.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)