Pages

SHIRIKA LA NYUMBA NHC LAZINDUA UUZAJI WA NYUMBA ZA MRADI WA 711 KAWE

k1
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia Mchechu Kyando akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa uuzaji wa nyumba za mradi wa 711 uliopo Kawe jijini Dar es salaam, Nyumba hizi ziko kwenye majengo 7 yenye ghorofa 11 kila moja ambayo yanatarajiwa kuchukua watu 1000 kwa na huu ni utangulizi wa ujenzi wa mji mpya wa kisasa unaotarajiwa kujengwa eneo la Tanganyika Pakers Kawe jijini Dar es salaam ambao ukikamilika utaweza kuchukua watu 15000.

Watu wanaohitaji kununua nyumba hizo wanatakiwa kufika ofisi za NHC Kinondoni au Makao Makuu ya Shirika la Nyumba NHC Upanga au wanaweza kutembelea kwenye mtandao wa shirika hilo kwa maelezo zaidi ili kununua nyumba hizo hafla ya uzinduzi wa nyumba hizo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika makao makuu ya shirika hilo Upanga.(PICHA NA JOHN BUKUKU WA FULLSHANGWE)
k4
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia Mchechu Kyando akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa uuzaji wa nyumba za mradi wa 711 uliopo Kawe jijini Dar es salaam. k17
Meneja wa Masoko na Mauzo wa NHC, Tuntufye Mwambusi akizungumza na Monica Joseph Mkurugenzi wa Kampuni ya Monifinace Investment Group Limited wakati wa uzinduzi huo.
k18
Meneja wa Masoko na Mauzo wa NHC, Tuntufye Mwambusi akimsikiliza Bw. David Shambwe Mkurugenzi wa Fedha Maendeleo ya Biashara NHC katika uzinduzi huo kulia ni Mwita Makenge Mkurugenzi wa Kampuni ya Wegmar Limited na kushoto ni William Genya Meneja Maendeleo ya Biashara NHC .
k19Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bw. Nehemia Mchechu katikati na Felix Maagi, Mkurugenzi wa Fedha wa NHC wakimsikiliza Linley Kapya kutoa Benki ya NBC wakati alipokuza akizungumza jambo katika uzinduzi huo.
k5
Meneja wa Masoko na Mauzo wa NHC, Tuntufye Mwambusi akizungumza na kuelezea jinsi mradi huo utakavyokuwa na mambo muhimu yaliyopo katika mradi huo huku akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa shirika hilo..
k06
Baadhi ya wafanyakzi wakipozi kwa picha w.akati wa hafla hiyo
k6
Meneja wa Masoko na Mauzo wa NHC, Tuntufye Mwambusi akifafanua jambo mbele ya waalikwa wakati alipokuwa akiuelezea mradi huo.
k07
Baadhi ya wageni walikwa wakifuatilia maelezo mbalimbali kuhusu mradi wa 711 wa Kawe jijini Dar es salaam.
k7
Meneja Masoko wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bw. Aden Kitomari akifafanua mambo mbalimbali wakati akiuelezea mradi wa 711 uliopo Kawe jijini Dar es salaam.
k08
Wageni waalikwa wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa na maofisa mbalimbali wa shirika la Nyumba NHC.
k8
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia Mchechu pamoja na wafanyakazi wa shirika hilo wakifuatilia video zilizokuwa zikionyesha jinsi mradi huo utakavyokuwa wakati wa uzinduzi uliofanyika Makao Mkuu wa shirika hilo Upanga.
k10
Baadhi ya wageni waalikwa kutoa taasisi mbalimbali wakifuatilia uzinduzi huo.
k12
Kutoka kulia ni Meneja wa Masoko na Mauzo wa NHC, Tuntufye Mwambusi na Meneja Masoko wa NHC Bw. Aden Kitomari wakimsikiliza Taji Liundi aliyekuwa MC wa uzinduzi huo.
k14 k15 k16
Wageni mbalimbali walihudhuraia uzinduzi huo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)