Pages

RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG AACHANA NA UKAPERA

 Bibi harusi Mary Michael Mbaya (kushoto), akimvisha pete ya ndoa mume wake Richard Mwaikenda ambaye ni mpiga picha mkuu wa gazeti la Jambo Leo na mmiliki wa Kamanda wa Matukio Blog, baada ya kubariki ndoa yao katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Kivule Dar es Salaam mchana huu.
 Bwana harusi Richard Mwaikenda akiwa amepozi na mke wake Mary Michael Mbaya wakati wa ibada yao ya ndoa.
 Mchungaji wa Kanisa hilo, Naory Chuma (kushoto), akiwabariki maharusi hao.
 Baba  wadogo wa bwana harusi Richard Mwaikenda wakiwa kwenye ibada hiyo.
 Wazazi wa bibi na bwana harusi wakiwa kwenye ibada hiyo. 
 Ndugu na jamaa wa maharusi hao wakiwa katika ibada hiyo.
 Hapa ni furaha tupu kwa ndugu wa maharusi.
 Maharusi hao wakiingia kanisani.
 Baadhi ya Waandishi wanaofanyakazi na bwana harusi wakijumuika katika ibada hiyo. Kutoka kushoto ni Peter Mwenda (Majira), Anicetus Mwesa, Said Mwishehe na Peter Ambilikile wote kutoka gazeti la Jambo Leo.
 Maharusi na wapambe wao wakiwa mbele ya kanisa.
 Wanandoa hao wakionesha shahada ya ndoa yao baada ya kukabidhiwa.
 Waumini wakiwa kwenye ibada hiyo.
 Maharusi hao wakitoka kanisani na wanandoa wenzao baada ya kufunga ndoa. Ndoa 11 zilifungwa katika kanisa hilo.
 Wanahabari wakiwa katika picha ya pamoja na maharusi hao.
Hapa ni furaha tupu. Wa tatu kulia ni mwanahabari, Nyakasagani Masenza.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)