Pages

Castle LITE yazindua nembo mpya inayotambulisha ubaridi wa kinywaji

Meneja wa bia ya Castle LITE nchini,Victoria Kimaro akitambulisha nembo mpya ya bia hiyo ikiwa baridi wakati hafla ya uzinduzi wake kwenye hafla iliyofanyika kwenye baa ya Break Point-Kinondoni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Baadhi ya wageni waliohudhuria hafla uzinduzi wa nembo mpya ya Castle LITE inayobadilika rangi na kuwa bluu inapokuwa kwenye ubaridi sahihi mpya ya kinywaji hicho  wakipatiwa maelezo juu ya mabadiliko hayo ya nembo .Hafla hiyo ilifanyika kwenye baa ya Break Point –Kinondoni jijini Dar es Salaam jana na kuhudhuriwa na wananchi kutoka sehemu mbalimbali za jiji 
 Baadhi ya wateja waliofika kwenye hafla ya uzinduzi wa nembo mpya ya bia ya Castle LITE inayobadilika rangi na kuwa bluu inapokuwa kwenye ubaridi sahihi   wakishindana kuweka mikono kwenye barafu wakiangaliwa na Meneja wa bia ya Castle LITE Tanzania ,Victoria Kimaro (kulia) wakati wa hafla ya uzinduzi na nembo hiyo ambapo ulikuwepo na michezo mbalimbali ya burudani iliyowawezesha washindi kujinyakulia zawadi mbalimbali.
 Meneja wa bia ya Castle LITE  ,Victoria Kimaro akiongea na waandishi wa habari wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi wa nembo.
 Baadhi ya maofisa wa Kampuni ya Bia Tanzania ( TBL) Kutoka kushoto ni Gareth Jones na Aidan Thomas  wakishindana kuweka mikono kwenye barafu wakati wa uzinduzi wa nembo mpya ya bia ya Castle LITE.  Hafla hiyo ya uzinduzi ilifanyika kwenye baa ya Break Point –Kinondoni jijini Dar es Salaam jana na kuhudhuriwa na wananchi kutoka sehemu mbalimbali za jiji

Dar es Salaam Desemba 5,2015:Castle Lite,bia namba  moja inayouzwa zaidi Tanzania imezindua nembo mpya ambayo inabadilika rangi na kuwa bluu pale inapokuwa kwenye ubaridi sahihi na kumfanya mtumiaji wa kinywaji hicho aifurahie inapokuwa kwenye ubaridi zaidi.

Uzinduzi  wa nembo hii yenye kuleta burudani ulifanyika mwishoni mwa wiki katika baa ya Break Point-Kinondoni na kuambatana na burudani na mashindano ambayo yaliwawezesha washindi kujinyakulia zawadi mbalimbali kutoka kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
 
Meneja wa Castle Lite,Victoria Kimaro alisema kuwa ubunifu huu ni wa aina yake na wa kwanza kufanyika nchini na lengo kubwa ni kuwapatia watumiaji wa kinywaji hiki burudani ya ziada  wanapokitumia kikiwa na kiwango cha ubaridi unaostahili.

“Pale nembo yenye hekalu inayopatikana kwenye chupa ya Castle Lite mpya inapobadilika na kuwa bluu,itaonyesha kwamba bia ya Castle LITE imapata ubaridi zaidi na kukufanya uburudike na kufurahia zaidi.Ubunifu huu ni mpya Tanzania na Afrika Mashariki na kutokana na ukanda huu kuwa wa joto,nembo hii mpya  itasaidia kumwonyesha mnywaji bia gani ina ubaridi zaidi”Alisema.

Wateja mbalimbali waliohudhuria uzinduzi huo na kuonja Castle Lite katika ubaridi unaostahili walisema kuwa nembo mpya itawasaidia kutambua  ubaridi wa kinywaji tofauti na ilivyokuwa hapo awali “Ubunifu huu ni wa aina yake kwa kuwa unatuwezesha kutambua ubaridi unaostahili wa bia wa kutazama nembo tofauti na ilivyokuwa hapo awali”Alisema Amandus Njau Mkazi wa Kinondoni mmoja wa wananchi waliohudhurua hafla hiyo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)