Na K-Vis Media/Khalfan Said
MFUKO wa Pensheni wa PPF, umeibuka kidedea kwa kutwaa tuzo ya uwasilishaji bora wa hesabu zake katika kipindi cha mwaka 2014.
Katika hafla ya kutoa tuzo kwa taasisi za serikali na za watu binafsi, Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu, NBAA, imetoa tuzo hizo kwa makampuni na taasisi mbalimbali nchini, ambapo kwa upande wa kundi la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, PPF ndiyo iliibuka ya kwanza ambapo Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko huo,
Bw. Martin Mmari kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu Bw. William Erio, alipokea tuzo hiyo kutoka kwa mgeni rasmi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Khamis Mwinyimvua. Pichani Bw. Mmari akipokea tuzo hiyo kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Khamisi Mwinyimvua. (Picha na K-Vis Media/Khalfan Said)

Bw. Khamisi akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na umuhimu wa kuwasilisha taarifa sahihi za hesabu
Bw. Mamri (wapili kulia), akigongesha glasi na mmoja wa waalikwa wakati wa hafla hiyo
Baadhi ya wawakilishi wa PPF katika hafla hiyo
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)