Yakiwa yamebaki masaa machache kuumaliza mwaka 2015 na kuukaribisha
mwaka mpya 2016 kwanza napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mwenyezi
Mungu muumba mbingu na nchi kwa neema na rehema zake kunifikisha hapa
nilipo leo nikiwa mzima wa afya na mwenye tumaini mbele zake.
Pia
nachukua nafasi hii kumshukuru Mungu wetu na baba yetu kwa mambo mengi
aliyotutendea na anayoendelea kututendea hakika si kwa uwezo wetu bali
ni kwa neema na rehema zake.
Namshukuru pia kwa kuweza
kunisimamia na kunipitisha kwenye majaribu ambayo kiukweli peke yangu
siyawezi lakini kwa msaada na uwepo wake amenisaidia kuyavuka na
kuyashinda mengi.
Tukikaribia kumaliza mwaka 2015 napenda
kuwashukuru kwanza Wazazi wangu kwa ushirikiano wao wote tokea mwaka huu
unaanza hadi leo tunapokaribia kuumaliza mwaka, vilevile niwashukuru
sana Dada zangu, kaka zangu kwa mazuri yao yote waliyonitendea hakika
bwana wetu na Mungu wetu atawaongezea maradufu pale mlipotoa. Nachukua
nafasi hii kuwashukuru marafiki zangu wa facebook, mtaani, ofisini na
popote pale kwa ushirikiano wenu mlionipa tokea mwanzo wa mwaka 2015
hadi leo tunaenda kuumaliza mwaka nawashukuru sana na mwenyezi Mungu
awatie nguvu, baraka na neema zake zipate kuwatembelea.
Nawashukuru pia wadau wote wa Lukaza blog ambao wameweza kufanya kazi na
sisi kuhakikisha lukaza blog inaendelea kung'ara ndani na nje ya nchi
na kuifanya Lukaza blog kufanikiwa kuibuka na Tunzo ya Blog Bora katika
Kipengele cha Siasa katika shindano la African Blogger Awards 2015
lililofanyika Afrika Kusini na lukaza blog kuwa mmoja wa washindi katika
kipengele kimoja wapo na kuufanya mwaka 2015 kuwa mwaka wa mafanikio
kwa Timu nzima ya Lukaza Blog ukiwemo na wewe msomaji wetu na mdau
wetu.Tunajipanga kuendelea kuwaletea mazuri zaidi kwa mwaka 2016.
Mwaka 2015 ulikua mwaka mgumu sana kwangu kutokana na kupitia majaribu
ambayo kwangu ni mazito sana na peke yangu siwezi kuyavuka lakini
naamini Kwa uwepo wake Rahabanah naamini leo ataenda kutenda miujiza
yake na kufanikisha kunivusha kwenye hili jaribu Kama ambavyo kila
jaribu huwa na mlango wa kutokea na Mungu wetu hampi mja wake jaribu
linalomzidi kimo au uwezo basi naamini jaribu hili naenda kulimaliza leo
mbele za bwana.Kikubwa ni kuwa na imani mbele zake huku tukiwa
wanyenyekevu mbele zake.
Napenda kuchukua nafasi hii kuwasamehe
wale wote walionikosea either kwa makusudi au bila hata kujua ili na
mimi mnisamehe wote niliowakosea kwa makusudi kabisa na hata wale
niliowakosea bila hata kujua kwa maana msamaha wenu kwangu ndio na mimi
nitaweza kusamehewa mbele ya Mungu wetu kwa kipimo kilekile ili kuweza
kuingia mwaka 2016 tukiwa na mioyo safi isiyokuwa na hata chembe za
hasira, masimango, chuki na uhasama.
Nachukua nafasi hii Kuendelea kuwashukuru wote na kuwasihi kuendelea na umoja, ushirikiano na kupendana
Nachukua nafasi hii kuwatakia watanzania wote na dunia nzima heri ya Mwaka mpya 2016.
Josephat Lukaza
Founder /Chief Editor
Lukaza Blog
http://www.josephatlukaza.com
Founder /Chief Editor
Lukaza Blog
http://www.josephatlukaza.com
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)