MKUU WA WILAYA AFANYA ZIARA YA KUKAGUA VYOO MANISPAA YA SHINYANGA..AKUTANA NA VYOO VYA AJABU...KIMO CHA KULENGA KWENYE BOMBA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MKUU WA WILAYA AFANYA ZIARA YA KUKAGUA VYOO MANISPAA YA SHINYANGA..AKUTANA NA VYOO VYA AJABU...KIMO CHA KULENGA KWENYE BOMBA



Hiki choo cha ajabu kiko Shinyanga maelezo yapo chini.Leo Jumatatu Novemba 30,2015 ambapo mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ameanza kufanya ziara kutembelea kata za manispaa hiyo ili kuangalia hali ya usafi wa mazingira kubwa zaidi ni kukagua vyoo vya wananchi ilimkukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu.Mkuu huyo wa wilaya ya Shinyanga alikuwa ameambatana na mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna,mwanasheria wa manispaa hiyo Simon Jilanga,afisa afya wa manispaa hiyo Heri Nakuzelwa,waandishi wa habari na askari wa jeshi la polisi.Mkuu huyo wa wilaya ametembelea kata ya Chibe na Kambarage na kubaini kuwa kaya nyingi hazina vyoo na kuagiza wajenge vyoo haraka huku akifunga maduka matano kutokana na kukosa vyoo.Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo kwenye msafara huo ametusogezea picha 37 kilichojiri....

Ziara ilianzia katika ofisi ya afisa mtendaji wa kata ya Chibe katika manispaa ya Shinyanga.Pichani ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro(mwenye kofia) akijiandaa kutembea mtaa kwa mtaa kukagua vyoo.Ziara ya mkuu huyo wa wilaya imekuja siku chache tu baada ya kufanya mkutano mkubwa na akina mama wa manispaa ya Shinyanga kujadili namna ya kupambana na ugonjwa wa kipindupindu ambapo mpaka sasa umeua watu watatu kati ya wagonjwa 98 waliripotiwa kukumbwa na ugonjwa huo unaotokana na mtu kula au kunywa kinyesi cha mtu mwingine baada ya kuingia kwenye maji au chakula.

Msafara wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ukielekea katika mtaa wa Chibe ambapo katika kata ya Chibe ina jumla ya kaya 1500 lakini kaya 398 hazina vyoo,lakini kati ya hizo kaya 1500 nyingi hazina vyoo bora

Mzee Jilili Njinya(kushoto) akijitetea kwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwanini hana choo katika familia yake na kuahidi kujenga ndani ya siku 7

Hii ni familia katika mtaa wa Chibe katika manispaa ya Shinyanga kulia ni choo cha familia hiyo



Familia ya Shija Kabakuli katika mtaa wa Chibe iliyopewa wiki moja ijenge choo kwani hawana choo na matokeo yake hujisaidia vichakani hali inayochangia kuwepo kwa ugonjwa wa kipindu pindu

Mwananchi akijitetea na kuahidi kujenga choo


Choo katika moja ya familia katika mtaa wa Chibe

Kushoto ni mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna,katikati ni afisa mtendaji wa kata ya Chibe Daniel Mtasibwa na mwandishi wa gazeti la Nipashe wakiwa katika mtaa wa Chibe kuangalia vyoo vya wananchi

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisikiliza maelezo kutoka kwa mtoto baada ya kuulizwa wazazi wake mbona hawaonekani nyumbani.....kumbe walikimbia baada ya kusikia kuna ukaguzi wa vyoo kutokana na familia hiyo kukosa choo na kulazimika kutumia choo cha jirani yao

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akitoa agizo kwa diwani wa kata ya Chibe John Kisandu juu ya familia ambazo hazina vyoo ambapo alitoa muda wa siku 7 wajenge vyoo na baada ya hapo atarudi kukagua

Waandishi wa habari wakishangaa choo cha aina yake...mchana hakitumiki kwa sababu hakina ukuta wala paa...yaani peupee....giza likiingia mtu anafanya yake

Choo katika familia mtaa wa Chibe kata ya Chibe manispaa ya Shinyang

Diwani wa kata ya Chibe John Kisandu akizungumza wakati wa ziara ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akikagua vyoo katika kata hiyo ambapo aliahidi kuhamasisha wananchi kujenga vyoo ili kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu

Diwani wa kata ya Chibe John Kisandu akionesha shimo la choo lililopo mbele ya familia...Shimo hilo liko wazi japokuwa limefunikwa kwa miiba,nzi wapo wa kutosha hali inayoweza kuchangia mlipuko wa ugonjwa kipindupindu

Diwani wa kata ya Chibe John Kisandu akimwagiza mama wa familia hiyo kufunika shimo la choo lililopo mbele ya familia hiyo ili kuepuka ugonjwa wa kipindupindu

Bibi hana wasiwasi....Choo changu kile paleeeeee!!

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro(kulia) akimweleza mwenyekiti wa mtaa wa Busambile bwana Charles Mayunga(mwenye kanzu) jinsi choo bora kinavyopaswa kuwa

Afisa afya wa manispaa ya Shinyanga(aliyevaa miwani) akiangalia shimo la choo kinachojengwa katika mtaa wa Busambile..ambapo alimtaka mama mwenye nyumba hiyo Severine Kulwa(katikati)kukamilisha ujenzi wa choo hicho haraka

Kushoto ni mwanasheria wa manispaa ya Shinyanga Simon Jilanga akimhoji kijana Sindi Fungwe kwanini hajajenga choo katika familia yake

Hapa ni Kata ya Kambarage-Pichani ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga akipokea maelezo kuhusu moja ya nyumba yenye wapangaji wengi ikiwa ni pamoja na ofisi ya serikali ya mtaa...Nyumba hiyo ni bora lakini hakuna choo

Muonekano wa nyumba hiyo isiyokuwa na choo bali bafu pekee kama linavyoonekana kulia likiwa na pazia la mifuko.Baada ya kusikia ugeni wa mkuu wa wilaya,mmiliki wa nyumba hiyo alitoweka

Muonekano wa mbele wa nyumba hiyo,ambapo mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro aliagiza maduka yaliyopo katika nyumba hiyo yafungwe mpaka pale watakapojenga choo

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akitafakari jambo katika mtaa wa Mwasele "A" wakati akikagua vyoo na kubaini kuwa katika mtaa huo ambao una kaya 22 zisizokuwa na vyoo na zenye vyoo vingi siyo bora

Muonekano wa choo katika familia moja mtaa wa Mwasele A kata ya Kambarage

Kijana akipika wakati wa ziara ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga katika mtaa wa Mwasele A ..pembeni kuna choo hakijafunikwa..angalia hapa chini

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages