MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA MTOTO WA KICHWA KIKUBWA NA MGONGO WAZI DUNIANI 2015 - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA MTOTO WA KICHWA KIKUBWA NA MGONGO WAZI DUNIANI 2015



 Meneja Ustawi wa Jamii na Mahusiano wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa ,Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Jumaa Almasi akizungumza kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi hiyo  Dk, Othman Kiloloma wakati wa  Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo wazi Duniani 2015, aliomba kuitumia siku hiyo kwa kusheherekea siku hiyo adhim amabayo nisiku maalum kwa sababu vijana wetu ambao tunawaongelea leo hi kwetu sisi ni wagonjwa kwa maana yakwamba Tiba yao yote kwa watoto wenye vichwa vikubwa  na  mgongo wazi Tiba yao  inapatikana katika Taasisi ya Mifupa Moi, sisi kwa kushirikiana na Chama cha Wazazi tunakuwa tukifanya kazi bila kuchoka na kwa pamoja kuhakikisha kwamba hawa watoto wanapata Tiba inayo stail kuhakikisha na wenyewe sikumoja watapata fulsa yakuwa viongozi na  kaulimbiu ya mwaka hu inasema PAMOJA TUZUIE  ULEMAVU WA KUZALIWA, kama tunavyo faham hawa watoto wanavyo zaliwa wanazaliwa na matatizo na hayo matatizo yanapelekea ulemavu na unakuwa mkubwa zaidi kama hawatapata tiba stahili kwa hiyo sisi kwa kushilikiana na Chama tunahakikisha kwamba hawa watotowanaletwa Hospitali wanapatiwa Tiba bure kwa hiyo na kuwashukuru wafadhili mbalimbali ambao wanajitolea kufanya kazi kwa pamoja na Taasisi hiyo, wapo wengi wanao saidia kama AHLAKUL-ISLAMU, akitowa wito  Jumaa Almasi, kuwaomba wazazi kuwaleta watoto ambao bado wanafichwa majumbani ambapo kwa Taasisi hiyo kwa mwaka hupokelewa watoto  400 hadi 500  kwa mwaka kwatakwimu walizonazo watoto 4000 kwa mwaka huzaliwa, nakuwasihi wazazi kuwa wao ni mashuhuda na kuona jinsi Wataalamu watiba wanavyo jitahidi kuwapatia tiba watoto hao.  (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA) Mmiliki wa UJIJIRAHAA BLOG
Mwenyekiti na Mjumbe wa Kamati ya kusaidia watoto wenye ulemavu wa vichwa vikubwa na mgongo wazi wakishirikiana na   WafanyaBiashara wa Sokoni Kariakoo Mtaa wa Raha Skweya  na Mhonda Jijini Dar es Salaam,  Ludovick Mmasi  akizungumza kwa niaba ya wenzake mara walipofika katika Maadhimisho hayo baada ya kuguswa na watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi  walipotembelea Taasisi hiyo ya Watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi na kujichangisha na kuwakilisha vitu mbalimbali kama, vyakula vya nafaka, Sabuni, pambas Mafuta  na kujitolea Damu   na kutowa wito kwa wengine waweze kujitolea kwa hali na mali kuungana kuisaidia Serikali na isiwe kuiachia kila kitu Serikali hata sisi Wananchi yatupasa kuguswa  tuisaidie Serikali yetu, Mwenyekiti huyo amesema wanakwenda  kujipaka na kusema watapeleka chakua kwa niaba ya Siku Kuu ya X-msa inayo karibia kwaniaba ya wafanyabiashara wenzake

 Mtoto Selemani Joseph (14) kushoto ambae ni mwanafunzi wa Darasa la Tatu katika Shule ya Mather Telesia iliyopo  Kisiwani, Kigamboni Dar es Salaam  akipozi na mwenzake katika ofisi za   Chama hicho cha wazizi kwa watoto  wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi wakati wakijiandaa kuanza maandamano



























 Wasanii wa Kikundi cha Sanaa cha Tuamke  cha Chanika Dar es Salaam  wakitoa burudani wakati wa Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongowazi yaliyofanyika kwenye viwanja vya  Taasisi ya Tiba ya Mifupa ,Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dar es Salaam




 Mlezi wa watoto hao na Muuguzi Kiongozi wa Wold ya Watoto hao katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Haulati Daud akiongea jambo wakati wa Maadhimisho hayo

 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Sikaungu Wilaya ya Sumbawanga, Mkoa wa Rukwa Filbert Nyakasi akitowa pongezi kwa waandaaji wa Maadhimisho hayo ambae anamtoto aliyekujanae na kulazwa katika Wodi ya watoto wavichwa vikubwa na mgongo wazi, ambapo mtoto wake anasumbuliwa na uvimbe unaosababisha  jicho la kulia kutoka nje, Mtoto wake anaitwa Angelina Malema (12), anaesoma Darasa la Nne Shule ya Msingi Mlanda 'A' Manispaa ya Sumbawanga, Kijiji cha Mlanda Mkoa wa Rukwa, Wilaya ya  Manispaa ya Sumbawanga  
 Mkurugenzi wa BM Saloon, Benno Chelele, akitoa zawadi katika Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kichwa kikubwa na Mgongowazi yaliyofanyika katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI), kwa niaba ya Dorcus Membe ambae alikuwa Mke wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe  na marafiki zake akiwa ndiye mlezi wa watoto hao






















No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages