Pages

IAWRT YAZINDUA RIPOTI YA NAFASI YA MWANAMKE KATIKA VYOMBO VYA HABARI

Bi Razia Mwawanga kutoka IAWRT akifungua mkutano wakati wa uzinduzi wa ripoti ya utafiti kuhusu wanawake wanavyopewa nafasi hasa katika vyombo vya habari hasa hapa nchini.(Picha na Geofrey Adroph wa Pamoja blog)
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali nchini la International Association of Women in Radio and Television (IAWRT) Tanzania Bi. Rose Haji Mwalimu akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa ripoti ya utafiti kuhusu wanawake wanavyopewa nafasi hasa katika vyombo vya habari hasa hapa nchini
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa TAMWA, Bi. Edda Sanga(kushoto) akiwahamasisha wanawake kuwa na uthubutu ili kuyafikia malengo waliyojiwekea na kutojiona hawawezi kisa wao ni watoto wa kike, kulia ni Mkurugenzi wa IAWRT Tanzania Bi. Rose Haji Mwalimu.

Mgeni rasmi Mkurugenzi wa TAMWA, Bi. Edda Sanga(kushoto) pamoja na Mkurugenzi washirika lisilo la kiserikali nchini la International Association of Women in Radio and Television (IAWRT) Tanzania Bi. Rose Haji Mwalimu wakizindua ripoti ya utafiti kuhusu mwanamke au mtoto wa kike anavyopewa nafasi hasa kwenye vyombo vya habari.




Wajumbe wa IAWRT wakiangalia moja ya filamu inayohusu nafasi ya mwanamke hasa katika jamii.




Wajumbe wa mkutano huo wakiendelea kutoa maoni yao kuhusu usawa wa kijinsia katika ngazi mbalimbali za maamuzi.

Picha ya pamoja. 

Na Mwandishi wetu 

Katika ripoti iliyotelewa awali na Shirika lisilo la kiserikali nchini la International Association of Women in Radio and Television Tanzania (IAWRT), imeonyesha kwamba wanawake au mtoto wa kike hapewi nafasi ya moja kwa moja katika kutoa taarifa au katika shughuli za kufanya maamuzi katika ngazi mbali mbali tofauti na watoto wa kiume au mwanaume.

Utafiti huo umebaini kwamba mbali na kutopewa mtoto wa kike nafasi ya kufanya maamuzi katika ngazi tofauti, ambapo wamesema inapelekea wanaume kupata kipato kikubwa zaidi ya wanawake.


Katika hafla hiyo mgeni rasmi alikuwa ni Mkurugenzi wa TAMWA, Bi. Edda Sanga, ambapo ameiomba serikali na vyombo vya habari kuwapa kipaumbele wanawake katika ngazi tofauti tofauti za uongozi ili kuweza kuondoa lile tabaka lililopo kati ya mwanamke na mwanaume, na pia inaweza kuchangia katika maendeleo na mabadiliko ya nchi kiujumla.

Aliongezea kwa kusisitizia kuwa wanawake wenyewe washirikiane na wajitume pale wanapopata fursa katika matukio, na pale wanapofanikiwa warudi kuja kusaidia kuinua wanawake wengine ambao bado hawajaweza kufika pale panapohitajika. 


Akizungumza Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali nchini la International Association of Women in Radio and Television (IAWRT) Tanzania, Bi. Rose Haji Mwalimu alisema kwa wanawake inabidi wajitambue na pia wajue thamani zao katika jamii ili waweze kufikia malengo yao.

Hayo aliyasema wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti kuhusu Mwanamke au mtoto wa kike anavyopewa nafasi hasa kwenye vyombo vya habari ambapo ilionekana mtoto wa kike hapewi nafasi sawa na mtoto wa kiume.


Hii imekuwa ni changamoto hasa kwa nchi za Afrika kutomthamini mtoto wa kike.

Pia lisisitiza kuwa licha ya juhudi nyingi za wanahabari na taasisi za habari kuwainua wanawake na wasichana katika vyombo vya habari mathalani Radio bado juhudi zinakabiliana na changamoto kadhaa licha ya kuzaa matunda kwa sehemu ndogo na kupelekea mwanaume kuwa na nafasi kubwa katika vyombo hivyo.


No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)