Pages

ENHANCE AUTO YAKABIDHI GARI KWA MSHIBNDI WA SHINDANO LA MATUMIZI BORA YA MITANDAO YA KIJAMII


Kamanda wa Kikosi Usalama barabarani, Mohamed Mpinga (kulia)
akimkabidhi zawadi ya gari aina ya Toyota Sarf, mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Jackson Kapongo aliyeshinda kupitia mchezo wa Matumizi bora ya Mitandao ya Kijamii iliyoendeshwa na Kampuni ya Enhance Auto ya Jijini Dar es  Salaam. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Enhance Auto, Aatif Farooq Butt.Picha na Father Kidevu Blog.
Mkurugenzi wa Enhance Auto, Aatif Farooq Butt akionesha stika za kuhamasisha usalama barabarani ambazo pia zilizinduliwa na Kamanda Mpinga.
 Meneja Mauzo Enhance Auto, Ayaka Kashida akionesha shindano jipya ambalo mshindi atajishindia Toyota Noah mpya. 
 Jackson Kapongo akiwa katika gari yake Toyota Sarf na pembeni yake ni Kamanda Mpinga. 
 
 Hii ndio gari jipya Toyota Sarf aliyo jishindia Kapongo. SOMA ZAIDI BOFYA HAPA

 Wageni mbalimbali waalikwa wakifuatilia tukio hilo.
 Bahati na sibu ilichezeshwa na wateja kujishindia mipira
Mkurugenzi wa Enhance Auto, Aatif Farooq Butta akitoa maelezo ya bahati nasibu ya kushinda mipira.
**************
Na Father Kidevu 


MHITIMU wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jackson Kapongo ameibuka mshindi na kukabidhiwa gari aina ya Toyota surf lenye thamani ya zaidi ya sh milioni 24 katika shindano lililochezeshwa na kampuni ya kuuza magari ya Enhance Auto.


Kapongo alikabidhiwa gari lake hilo na Kamanda wa Polisi Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga baada ya kushinda katika shindano lililoendeshwa na Enhance Auto likiwataka washiriki kuonesha ni namna gani  wanaweza kutumia mitandao ya kijamii na kujiletea manufaa.


Akizungumza kampuni hiyo, Mpinga alisema imekuwa ikichezesha shindano hilo kila mwaka na kushirikisha nchi mbalimbali Afrika ambapo kwa mwaka jana mshindi alipatikana kutoka Zambia lakini kwa mwaka huu ameshinda mtanzania hivyo ni jambo la kujivunia.


Alisema mbali na kutoa zawadi lakini kampuni hizo za magari zinajukumu kubwa la kutoa mchango kwa usalama barabarani kwa kutoa elimu sambamba na kuuza magari yenye viwango vinavyokubalika ili kuepusha ajali zisizo za lazima.


"Natoa wito kwa kampuni zingine kuwekeza katika usalama barabarani na wasifikirie tu kuuza magari bali wahakikishe magari yanakuwa salama na wanaoendesha wanakuwa salama... tuagize magari yenye viwango mana ajali nyingi pia zinasababishwa na ubovu wa magari" alisema.


Mapema Mkurugenzi wa Enhance Auto, Aatif Farooq Butt alisema shindano hilo mshiriki anatakiwa kushiriki kwa kuchagua mitandao yao ya kijamii kwa wingi zaidi na lilishirikisha nchi ambazo wanafanya nao  biashara ikiwemo Botswana, Burundi, Jamhuri ya Kongo, Malawi, Msumbiji, Sudan ya Kusini,  Uganda, Zambia, Zimbabwe na Tanzania.


Hata hivyo alisema kwa kutambua umuhimu wa usalama barabarani kwa kushirikiana na jeshi la polisi kikosi cha Usalama Barabarani  wameanzisha kampeni ya 'Endesha kwa Usalama' ambapo pia walikabidhi stika za magari lengo likiwa ni kujenga uhusiano na wateja wao.


Akizungumza zawadi hiyo, Kapongo aliishukuru kampuni hiyo na kuwataka vijana kutumia mitandao ya kijamii kwa faida na si kwa kujifunza mambo ambayo huharibu maadili ya jamii.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)