Meneja wa bia ya Castle LITE nchini,Victoria Kimaro
akitambulisha nembo mpya ya bia hiyo ikiwa baridi wakati hafla ya uzinduzi wake
kwenye hafla iliyofanyika kwenye baa ya Break Point-Kinondoni jijini Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wageni waliohudhuria hafla uzinduzi wa nembo mpya ya Castle LITE inayobadilika rangi na kuwa bluu inapokuwa kwenye ubaridi sahihi mpya ya kinywaji hicho wakipatiwa maelezo juu ya mabadiliko hayo ya nembo .Hafla hiyo ilifanyika kwenye baa ya Break Point –Kinondoni jijini Dar es Salaam jana na kuhudhuriwa na wananchi kutoka sehemu mbalimbali za jiji
Baadhi ya wateja waliofika kwenye hafla ya uzinduzi wa nembo mpya ya bia ya Castle LITE inayobadilika rangi na kuwa bluu inapokuwa kwenye ubaridi sahihi wakishindana kuweka mikono kwenye barafu wakiangaliwa na Meneja wa bia ya Castle LITE Tanzania ,Victoria Kimaro (kulia) wakati wa hafla ya uzinduzi na nembo hiyo ambapo ulikuwepo na michezo mbalimbali ya burudani iliyowawezesha washindi kujinyakulia zawadi mbalimbali.
Meneja wa bia ya Castle LITE ,Victoria Kimaro akiongea na waandishi wa habari wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi wa nembo.
Baadhi ya maofisa wa Kampuni ya Bia Tanzania ( TBL) Kutoka kushoto ni Gareth Jones na Aidan Thomas wakishindana kuweka mikono kwenye barafu wakati wa uzinduzi wa nembo mpya ya bia ya Castle LITE. Hafla hiyo ya uzinduzi ilifanyika kwenye baa ya Break Point –Kinondoni jijini Dar es Salaam jana na kuhudhuriwa na wananchi kutoka sehemu mbalimbali za jiji
Dar es Salaam Desemba
5,2015:Castle
Lite,bia namba moja inayouzwa zaidi
Tanzania imezindua nembo mpya ambayo inabadilika rangi na kuwa bluu pale
inapokuwa kwenye ubaridi sahihi na kumfanya mtumiaji wa kinywaji hicho
aifurahie inapokuwa kwenye ubaridi zaidi.
Uzinduzi wa nembo hii
yenye kuleta burudani ulifanyika mwishoni mwa wiki katika baa ya Break
Point-Kinondoni na kuambatana na burudani na mashindano ambayo yaliwawezesha
washindi kujinyakulia zawadi mbalimbali kutoka kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
Meneja wa Castle Lite,Victoria Kimaro alisema kuwa ubunifu
huu ni wa aina yake na wa kwanza kufanyika nchini na lengo kubwa ni kuwapatia
watumiaji wa kinywaji hiki burudani ya ziada
wanapokitumia kikiwa na kiwango cha ubaridi unaostahili.
“Pale nembo yenye hekalu inayopatikana kwenye chupa ya Castle
Lite mpya inapobadilika na kuwa bluu,itaonyesha kwamba bia ya Castle LITE
imapata ubaridi zaidi na kukufanya uburudike na kufurahia zaidi.Ubunifu huu ni
mpya Tanzania na Afrika Mashariki na kutokana na ukanda huu kuwa wa joto,nembo
hii mpya itasaidia kumwonyesha mnywaji
bia gani ina ubaridi zaidi”Alisema.
Wateja mbalimbali waliohudhuria uzinduzi huo na kuonja Castle
Lite katika ubaridi unaostahili walisema kuwa nembo mpya itawasaidia
kutambua ubaridi wa kinywaji tofauti na
ilivyokuwa hapo awali “Ubunifu huu ni wa aina yake kwa kuwa unatuwezesha
kutambua ubaridi unaostahili wa bia wa kutazama nembo tofauti na ilivyokuwa
hapo awali”Alisema Amandus Njau Mkazi wa Kinondoni mmoja wa wananchi
waliohudhurua hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)