Sehemu ambako utaanzia upanuzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco jijini Dar es salaam yenye urefu wa kilometa 4.3 kwa kuongeza njia mbili za barabara za lami kufuatia agizo la Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli la kutumia fedha shilingi bilioni nne zilizopaswa kutumika kugharamia Shamrashamra za siku ya Uhuru Desemba 9, 2015 kutumika kufanya upanuzi wa barabara hiyo. PICHA NA IKULU
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameamuru fedha zilizopaswa
kutumika kugharamia shamra shamra za siku ya Uhuru ambazo zingefanyika tarehe
09 Desemba 2015, kutumika kufanya upanuzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco jijini Dar es Salaam yenye urefu wa kilometa 4.3 kwa
kuongeza njia mbili za barabara za lami.
Tayari fedha hizo kiasi
cha shilingi bilioni nne zimepelekwa kwa wakala wa barabara hapa nchini
TANROADS kwa ajili ya utekelezaji wa agizo hilo, linalopaswa kuanza mara moja
Akizungumza na Mtendaji
Mkuu wa TANROADS Mhandisi PATRICK MFUGALE Ikulu Jijini Dar es Salaam, Dkt.
Magufuli ametaka ujenzi wa barabara hiyo uanze haraka ili kukabiliana na adha
ya msongamano wa magari katika barabara
hiyo
Kujengwa kwa njia hizo
kutaifanya barabara ya Morroco hadi Mwenge kuwa na njia tano.
Wakati huo huo, Rais
John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti Mstaafu wa Chama
Cha wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba Ikulu Jijini Dar es salaam.
Katika Mazungumzo hayo
Prof. Lipumba amempongeza Dkt. Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa awamu ya
tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na pia kwa kutoa hotuba nzuri ya
uzinduzi wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyokonga nyoyo za
Watanzania.
Kwa Upande wake Rais
Magufuli amempongeza Prof. Lipumba kwa msimamo wake thabiti wa kupinga ufisadi
na amemtakia heri katika shughuli zake.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es Salaam.
30
Novemba,2015
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)