Job Ndugai ndie spika mpya wa bunge la 11 la bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Job Ndugai ndie spika mpya wa bunge la 11 la bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania

Hatimaye Job Yustino Ndugai CCM amechaguliwa kuwa Spika wa bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuchaguliwa kwa kura 254 sawa na
asilimia 70% ya kura zilizopigwa akifuatiwa na mgombea wa CHADEMA
Goodluck Ole Medeye ambaye amepata kura 109.

Hata hivyo wagombea  hao ambao walikuwa 7 kati ya 8 wameweza kutoa shukrani na pongezi kwa  Ndugai wakisema anastahili na ndio maana akachaguliwa na kumtaka aongoze vyema bunge hilo.

 Job Ndugai ameibuka mshindi wa kiti cha Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupata kura 254 sawa na asilimia 70 ya kura zote ambapo jumla ya kura zilizopigwa ni 365

Matokeo ya kura za Spika.

A: Job Ndugai (CCM)- 254
B: Goodluck Ole Medeye (CHADEMA) - 109
C: Hashimu Rungwe (CHAUMA)- 0
D: Peter Sarungi (AFP) -0
E: Dkt Godfrey Malisa (CCK)- 0


F: Richard Lymo (T.L.P) -0
G: Robert Kisinini (DP) -0


Kura zilizoharibika ni 2

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages