Wanamuziki Ben Paul na Fid Q wanaoshiriki kwenye onyesho la Coke Studio wakiwa katika picha ya pamoja na washabiki wao wakati wa uzinduzi wa onyesho hili jijini Dar es Salaam hivi karibuni
Sehemu ya wafanyakazi wa kiwanda cha Coca Cola Kwanza wakifuatilia onyesho la Coke Studio
Msimu wa Coke Studio umewahusisha pia wanafunzi mashuleni kuonyesha vipaji vyao kama anavyoonekana mwanafunzi akionyesha kipaji cha kucheza katika moja ya tamasha la Coke Studio lililofanyika mjini Mwanza hivi karibuni
Mwanamuziki nguli wa Bongo Fleva
nchini Ben Paul amesema kuwa ushiriki wake katika onyesho la Coke Studio ni
moja ya mafanikio katika safari yake ya muziki.
Katika mahojiano aliyoyafanya wiki
hii kuhusiana na ushiriki wake katika onyesho hili maarufu linaloendeshwa na
kampuni ya Coca-Cola na kushirikisha kolabo za wanamuziki mbalimbali wa Tanzania
na nje ya nchi alisema anajivunia ushiriki wake katika onyesho hili na ameweza
kujifunza mengi kuhusiana na fani ya muziki.
“Japo hapo awali nimewahi kushinda
tuzo mbalimbali za muziki lakini ushiriki wangu katika onyesho hili kubwa la kimataifa ni moja ya mafanikio yangu
makubwa katika safari yangu ya muziki.
Alisema anajisikia fahari kufanya kolabo kwa kushirikiana na
mwanamuziki Wangechi kutoka nchini Kenya katika msimu huu wa Coke Studio ambapo
kwa hapa nchini onyesho hilo linarushwa kila siku ya Jumamosi saa kumi na mbili
jioni kupitia luninga ya Clouds.
Ben Paul alisema onyesho la Coke
Studio linahamasisha vijana kujiamini na kuonyesha vipaji vyao na aliwataka
vijana wenzake kujiamini na kutokata tamaa iwapo wanataka kutimiza ndoto zao na
kufanikiwa katika maisha.
Alisema katika safari yake ya muziki
amekutana na changamoto nyingi mojawapo ikiwa ni kunyimwa nafasi ya kurekodi
nyimbo zake na waandaaji mbalimbali wakiamini kuwa hakuwa na uwezo wa kuimba
lakini licha ya kufanyiwa hivyo aliendelea kupambana mpaka kufanikiwa kufika
alipo sasa.
“Ninachotaka kuwaambia ni kwamba,
mfano, kwa wale wenye vipaji vya kuimba, kitu kikubwa unachotakiwa kufanya ni
kuwa na nyimbo nyingi ambazo, hata ukirekodi moja isipofanya vizuri, unatoa
nyingine ili kuhakikisha unaendelea kusikika masikioni kwa watu”, alisema
Aliwaasa vijana wa jinsia zote kujiamini na kuondokana na dhana kwamba jinsia
fulani ndio wanaweza kufanya kitu fulani
na kusisitiza kuwa kila mtu ana kipaji na anaweza kufanya mambo makubwa.
Alimalizia kwa kuwapongeza wanamuziki
wenzake kutoka Tanzania ambao wako nao katika msimu huu wa tatu wa Coke Studio
mwaka huu. Wanamuziki hao ni Fid Q ambaye amefanya kolabo (mash-up) na Maurice
Kirya na Vanessa Mdee ambaye amefanya kolabo (mash-up) na mwanamuziki 2face
kutoka Nigeria na Ali Kiba ambaye amefanya Kolabo na mwanamuziki Victoria Kimani.
Lengo kuu la Coke Studio Afrika ni
kuwakutanisha kwa pamoja wasanii wenye mbalimbali wa Afrika na kuimba nyimbo
ambazo zina vionjo tofauti hivyo kuongeza msisimuko. Lakini vilevile kutoa
fursa kwa wasanii wachanga kushirikiana
na wasanii wakubwa ili kuwapa changamoto ya kuongeza ujuzi katika kazi zao na
kuzidi kukuza vipaji vyao
Onyesho la Coke Studio linarushwa
kila siku ya Jumamosi saa kumi na mbili jioni kupitia luninga ya Clouds. Pia
unaweza kusikiliza kipindi cha Coke Studio kwenye Clouds FM kila Jumamosi saa
nne asubuhi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)