Ardhi yapasuka na kumeza magari 12 - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Ardhi yapasuka na kumeza magari 12


Mississipi
Image captionHakuna aliyejeruhiwa katika kisa hicho
Wataalamu wa jiolojia wameitwa kuchunguzwa ni jinsi gani ardhi ilipasuka na kumeza magari 12 katika maegesho ya magari jijini Mississippi.
Shimo kubwa, la urefu wa futi 400 (120m) na upana wa futi 35 (11m), lilitokea baadaye Jumamosi katika eneo la Meridian, karibu na barabara kuu ya Alabama.
Eneo hilo limekuwa likipokea mvua kubwa katika kipindi cha wiki mbili zilizopita, kwa mujbiu wa gazeti la Meridian Star.
Hakuna aliyejeruhiwa katika kisa hicho, na wahandisi wanatarajiwa kudadisi uthabiti wa ardhi eneo hilo leo.
Bw Buck Roberts, tmkurugenzi wa usalama wa umma eneo la Meridian, aliambia gazeti hilo kwamba hilo halionekani kuwa shimo la kawaida ambalo hutokana na sehemu inayohifadhi maji chini ya ardhi kukauka na ardhi kuporomoka.Chanzo BBC Swahili

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages