Pages

Washindi wa Shindano la 'Genius-Cup' Wazawadiwa

Mwanafunzi Fuad Thabit kutoka Feza Boys Secondary aliyeibuka mshindi wa kwanza shule za sekondari katika Shindano la Genius-Cup akipokea cheti na zawadi yake ya shilingi 300,000 toka kwa  mgeni rasmi wa hafla hiyo, Ofisa Mkuu  wa Utafiti taasisi ya COSTECH, Athman Mgumia.
Wanafunzi Sita Washindi wa Shindano la Genius-Cup (mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na vyeti vyao mara baada ya kuibuka washindi. Nyuma yao ni meza kuu katika hafla ya kuwazawadia ikipata picha ya ukumbusho na mabingwa hao. 
Mkurugenzi wa Shule za Fedha Tanzania akizungumza katika hafla ya kuwazawadia washindi wa shindano la Genius-Cup.
Baadhi ya wanafunzi walioingia fainali katika shindano la kuwatafuta washindi wa shindano la Genius-Cup wakifuatilia hafla hiyo jana.
Ofisa Mkuu wa Idara ya Elimu kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Fredrick Shuma akizungumza katika hafla ya shindano la Genius-Cup jana.
Baadhi ya walimu na wazazi waliowaleta washiriki na kufanikisha ushindi wao wakiwa katika hafla hiyo jana.
Mgeni rasmi katika hafla ya kuwazawadia washindi wa Shindano la Genius-Cup mgeni rasmi wa hafla hiyo, Ofisa Mkuu  wa Utafiti taasisi ya COSTECH, Athman Mgumia (wa pili kulia)  akiwa na viongozi wengine wa meaza kuu. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Feza, Ibrahim Yunus.
Burudani toka kwa wanafunzi ikiendelea...!
Mmoja wa wanafunzi washindi wa shindano la Genius-Cup (kushoto) akipongezwa mara baada ya kupokea cheti na zawadi yake.
Mwanafunzi Shammah Kiunsi (kushoto) wa shule za msingi Mkoa wa Mbeya aliyeibuka msindi wa pili na kujishindia kitita cha shilingi 200,000 akipokea cheti na zawadi yake toka kwa mgeni rasmi katika hafla ya shindano la Genius-Cup jana.
Mmoja wa washindi katika shindano la Genius-Cup, Fuad Thabit (katikati) ambaye ni mshindi wa kwanza kutoka Feza Boys Secondary akipiga picha na viongozi wa meza kuu katika hafla hiyo jana.
WANAFUNZI Sita walioibuka mabingwa wa Shindano la Genius-Cup la masomo ya sayansi na hisabati wamezawadiwa zawadi zao jana katika fainali za mashindano hayo zilizofanyika katika Shule ya Wavulana ya Feza Sekondari iliyopo Tegeta Jijini Dar es Salaam.

Shindano hilo lililoshindanisha shule mbalimbali za msingi na sekondari nchini Tanzania na kuratibiwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kushirikiana na uongozi wa Shule za Feza nchini limejumuisha zaidi ya wanafunzi 1,486 limelenga kukuza vipaji vya wanafunzi hasa masomo ya sayansi na hisabati.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mara baada ya kumalizika kwa shindano hili, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Feza, Ibrahim Yunus alisema wanafunzi sita walioibuka washindi na kupatia vitita vya fedha ni pamoja na Fuad Thabit mshindi wa kwanza kutoka Feza Boys Secondary aliyejipatia shilingi 300,000 na Zulfa Khamis msindi wa pili toka shule za sekondari Mkoani Tanga aliyejishindia shilingi 200,000.

Bw. Yunus alimtaja mshindi mwingine wa kwanza shule za msingi ni Mvano Michael Cabangoh kutoka shule ya Green Acres aliyejishindia shilingi 300,000 na Shammah Kiunsi mwanafunzi wa shule ya msingi kutoka Mkoa wa Mbeya aliyejishindia kitita cha shilingi 200,000 pamoja na Dorice Ernest Msafiri mshindi wa tatu (msingi) kutoka Mkoa wa Dodoma Ignatius School aliyejinyakulia shilingi 150,000/-.

Akifafanua zaidi Mwalimu Mkuu wa Sekondari ya Wavulana ya Feza, Bw. Yunus alisema wanafunzi walioingia fainali na kukutanishwa kwa pamoja ni 70 kati ya wanafunzi 1,486 walioshiriki katika kinyang'anyiro hicho. Aliongeza kuwa hii ni mara ya pili shindano la GENIUS CUP linafanyika kwani kwa mara ya kwanza lilifanyika mwaka jana huku likilenga kukuza mapenzi ya masomo ya sayansi na hisabati kwa wanafunzi wa Tanzania.

Kwa upande wake Ofisa Mkuu wa Idara ya Elimu kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Fredrick Shuma akizungumza kabla ya kukabidhi vyeti kwa wanafunzi washindi aliupongeza uongozi wa shule za fedha nchini kwa kuliendeldeza shindano hilo kwani linachangia kuleta chachu ya mapenzi kwa masomo ya sayansi na hisabati kwa wanafunzi nchini Tanzania ambao wamekuwa wakiyaogopa masomo ya sayansi.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)