Taasisi ya fedha ya FAIDIKA wazindua huduma mpya ya ‘Faidika na Samsung Tabs' kwa wateja wa Dar - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Taasisi ya fedha ya FAIDIKA wazindua huduma mpya ya ‘Faidika na Samsung Tabs' kwa wateja wa Dar

DSC_2594
Ofisa Mtendaji mpya wa Faidika, Bw. Mbuso Dlamini wa pilikutoka kushoto akiwa sambamba na Meneja matekeleo wa taasisi hiyo, Haruna Feruzi wakiwa wameshika moja ya Samsung galaxy tab ambazo watakuwa wanakopesha wateja wao kuanzia sasa. Wanaofuatia ni Meneja wa kitengo cha Mauzo SME, kutoka kampuni ya AIRTEL, Bw. Killian Nango akishikilia bidhaa hizo pamoja na Meneja wa Samsung, Bw. Payton Kwembe. Wakionesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Andrew Chale wa modewjiblog).
Na Mwandishi Wetu
[DAR ES SALAAM]. Taasisi ya fedha ya FAIDIKA imezindua huduma mpya ya mikopo itakayowezesha wateja wake wa Dar es salaam kujipatia simu za kisasa za tableti kutoka kampuni ya Samsung ikiwa ni pamoja na muda wa matumizi wa data za 3GB kutoka mtandao wa AIRTEL.
Taasisi hiyo ambayo kwa sasa inatoa mikopo kwa wafanyakazi wa serikali na watumishi wa umma wanatoa mikopo mipya hiyo kwa kushirikiana na kampuni ya Samsung na Airtel ilikuwezaa wateja wao hao kwenda na wakati wa tehama.
Wakizindua huduma hiyo mpya leo Oktoba 8.2015 mbele ya waandishi wa habari, inayojulikana kama ‘FAIDIKA na SAMSUNG TAB' imelenga kuwawezesha kiurahisi kwa njia ya mkopo kupata SAMSUNG GALAXY TABS, na data za ukubwa wa 3GB kutoka AIRTEL.
DSC_2589
Ofisa Mtendaji mpya wa Faidika, Bw. Mbuso Dlamini (wa pili kutoka kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya taasisi hiyo ya kifedha inayojishughulisha na ukopeshaji nchini na nchi mbalimbali barani Afrika.
Akizungumza na waandishi wa habari Ofisa Mtendaji mpya wa Faidika Mbuso Dlamini amesema kwamba huduma hiyo mpya imelenga kuwasaidia wateja wao kuwa na uwezo wa kupata taarifa mbalimbali kupitia Tehama na hali ya kisasa katika kuboresha shughuli za kila siku.
Ameeleza kwamba huduma hiyo itatolewa kwa awamu mbalimbali na kwa kuanzia sasa wanaitoa kwa wateja wa Mkoa wa Dare s salaam na baadae wataendelea katika mikoa mingine katika matawi yao yote yaliyopo nchini nzima.
“Huduma yetu ya ‘FAIDIKA na SAMSUNG TAB' itawawezesha wafanyakazi wengi wa serikali kuboresha mfumo wao wa maisha kwa kuwa na uwezo wa kupata taarifa mbalimbali kwa njia ya tehama” amesema Bw. Dlamini.
Watu wanaohitaji mkopo huo utafanyiwa kazi katika muda wa saa 48 kwa wateja watakaokidhi vigezo na masharti ya FAIDIKA kama wanavyokopa katika mikopo mingine ya taasisi hiyo.
DSC_2544
Meneja matekelezo wa FAIDIKA, Haruna Feruzi akielezea jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya mikopo hiyo inavyotolewa ambapo mteja pindi atakapokopa namna ya ulipaji na njia ya kufuata ilikupata mkopo huo. Anayemfuatia ni Ofisa Mtendaji mpya wa Faidika, Bw. Mbuso Dlamini
Naye Meneja matekelezo wa FAIDIKA, Haruna Feruzi amesema wateja wote wa ‘FAIDIKA na SAMSUNG TAB' watatakiwa kuwasilisha hati za malipo yao ya mishahara ya miezi miwili, taarifa za benki kwa miezi miwili kitambulisho na picha moja ya pasipoti ili kupata mkopo huo.
“Nia yetu ni kuona kwamba tunaboresha kiwango cha maisha cha watanzania kwa kuwapatia fedha na teknolojia,” alisema Bw. Feruzi.
DSC_2560
Meneja wa kitengo cha Mauzo SME, kutoka kampuni ya AIRTEL, Bw. Killian Nango akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya mtandao huo utakavyorahisha huduma mbalimbali za mawasiliano na tehema kwa wateja wa FAIDIKA watakaopata mikopo ya Samsung tab. Kulia kwake ni Meneja wa Samsung, Payton Kwembe.
Akiongea kuhusu ushirika huo, Meneja wa Kitengo cha wateja wa makampuni madogo wa Airtel, Meneja Mauzo wa kitengo cha SME, Killian Nango alipongeza ushirikiano huo kwani utasaidia kuboresha zaidi maisha ya wateja wanaopata mikopo ya kifedha katika FAIDIKA na kwendana na wakati katika dhana ya tehama.
“Ushirika huu unaenda sambamba na dhamira yetu ya kutoa huduma za kibunifu zinazoendana na simu za kisasa ilikuwapatia wateja wetu uzoefu bora wa mawasiliano wakati wote. Tunayofuraha kwa kupitia ushiriikiano huu kati yetu na FAIDIKA na Samsung kutawezesha wateja wetu kupata simu za kisasa na kuunganishwa kifurushi cha intaneti cha 3GB kwa muda wa miezi mitatu pale watakaponunua simu zao.
Tunaamini watakaofaidika na mpango huu wa kupaata simu za kisasa za Samsung watafurahia huduma zetu za intaneti iliyo bora, ya haraka na bei nafuu” alieleza Killian Nango katika mkutano huo.
DSC_2570Meneja bidhaa wa Samsung, Bw. Payton Kwembe akielezea jambo juu ya bidhaa zao hizo na ubora wake kwa waandishi wa habari (hawapo pichani). Kushoto kwake ni Meneja wa kitengo cha Mauzo SME, kutoka kampuni ya AIRTEL, Bw. Killian Nango.
Kwa upande wake Meneja bidhaa wa Samsung, Bw. Payton Kwembe alibainisha kuwa, simu hizo za kisasa za SAMSUNG GALAXY TABS, ni miongoni mwa simu bora na zinazoongoza katika soko la bidhaa za kisasa hasa katika utendaji wake wa kazi.
“Samsung Galaxy TAB ni bidhaa za kisasa na zenye uwezo mkubwa wa utendaji wa kazi. Mteja atakapokuwa nayo hii itamwezesha pia kufanya shughuli zake za kiofisi na majukumu yake mengine kwa urahisi maahala popote pale na itamrahisishia shughuli zake.” Amebainisha Bw. Kwembe.
KUHUSU FAIDIKA.
FAIDIKA ni moja ya makampuni ya Letshego Holdings Limited. Letshego imesajiliwa mwaka 1998 mjini Gaborone, Botswana na kuorodheshwa katika Botswana Stock Exchange (BSE) mwaka 2002.
Ni kampuni mama yenye makampuni yanayojihusisha na ukopeshaji na uwekezaji katika nchi tisa za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika ikiwemo nchi za Botswana, Kenya, Lesotho, Msumbiji, Namibia, Rwanda, Swaziland, Tanzania na Uganda.
Letshego ni kampuni kubwa ya kizalendo iliyosajiliwa katika soko la hisa la Botswana (BSE) ikiwa na mtaji wa zaidi ya dola za Marekani milioni 700 na faida ya zaidi ya dola za Marekani milioni 97 kabla ya kodi, kwa mwaka 2014.
Kampuni ni miongoni mwa makampuni bora 30 yaliyopo Kusini mwa Jangwa la Sahara, ukiachia taifa la Afrika Kusini.
DSC_2549
Ofisa Mtendaji aliyemnaliza muda wake Bi. Marion Moore,(katikati) akifuatilia kwa makini uzinduzi huoakifuatiwa na wageni wengine pamoja na waandishi wa habari katika uzinduzi huo uliofanyika katika ofisi za taasisi hiyo jijini Dar es Salaam-Tanzania.
FAIDIKA Tanzania:
Nchini Tanzania, LETSHEGO inafanyakazi kwa kupitia FAIDIKA. Kampuni hii iliingia nchini mwaka 2006 na toka wakati huo imekuwa na jina lenye mafanikio makubwa. Shughuli za kampuni ya Faidika zimeenea karibu Tanzania nzima, huduma zake zikitolewa katika vituo 105 na maofisa 230 wanaowezesha huduma zake.
Faidika inafanya kazi zake kwa kuangalia namna nzuri ya utoaji wa huduma za fedha kwa kumwezesha mtaka huduma kuelewa vyema kuhusu mahitaji yake hasa matumizi ya mikopo yake kwa ubunifu na umakini, utoaji wa elimu ya fedha kwa wateja na jamii na kuwawezesha wasiokuwa na uwezo kuwa nao ili waweze kujipatia maisha bora.
Kupitia wateja zaidi ya 50,000. FAIDIKA imefanikiwa kuboresha maisha ya watanzania zaidi ya Laki tatu. Utafiti wa kisoko uliofanywa na taasisi hiyo, umeonesha kwamba asilimia 60 ya huduma zitolewazo za kifedha zinatumika kwa namna bora kabisa katika ujenzi, biashara, elimu na uwekezaji.
FAIDIKA inaendelea na itaendelea na safari ya kufikia hatua ya juu zaidi na wateja wao kuhakikisha kwamba wanatekeleza ahadi yao ya kuboresha maisha ya wananchi.
DSC_2534
Ofisa wa FAIDIKA, Andrew Okkalo akitoa maelezo juu ya kampuni kwa wandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa uzinduzi huo wa huduma hiyo mpya.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages