Pages

RAIS KIKWETE ATOA HESHIMA ZAKE ZA MWISHO KWA MAREHEMU DEO FILIKUNJOMBE NA WENZAKE WAWILI WALIOFARIKI KATIKA AJALI YA HELIKOPTA

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgombea Urais wa tiketi ya CCM Dkt.John Pimbe Magufuli wakitoa heshima za mwisho mbele ya majeneza ya aliyekuwa Mbunge wa Ludewa(CCM) Marehemu Deo Filikunjombe na wenzake wawili waliofariki katika ajali ya helikopta juzi katika pori la akiba la mbuga ya Selous. Marehemu aliagwa katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Mke wa Marehemu Bi Sarah Filikunjombe wakati wa kuaga mwili wa marehemu katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015. ( Picha na Freddy Maro )

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)