Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akizungumza na waandi wa habari wapo picha juu ya ujenzi wa bandari ya Bagamoyo utakaokuwa wa aina yake Afrika Mashariki na Kati, unatarajiwa kugharimu dola za Marekani bilioni 10 na kukamilika kati ya miaka mitano hadi saba ijayo. kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa CMHI ambaye pia ni Makamu wa Rais Mtendaji wa kampuni ya China Merchant Group Dk Hu Jianhua.kikao hichi kimefanyika leo jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbarimbari na Mjumbe kutoka China Mkurugenzi Mtendaji wa CMHI ambaye pia ni Makamu wa Rais Mtendaji wa kampuni ya China Merchant Group Dk Hu Jianhua.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe amewathibitishia wakazi wa Bagamoyo kuwa wale wote watakaoguswa na mradi wa ujenzi wa bandari mpya watalipwa fidia na wengine watajengewa nyumba kwenye maeneo ya mji huo.
Akizungumza na wandishi wa habari badaa ya kukutana na Mkurugenzi wa Kampuni ya China Merchants Group itakayosimamia ujenzi huo, Dk Hu Jianhao, Membe alisema katika ujenzi huo utakaochukua hekta 2400, wananchi wote watakaohuswa hawataachwa bure.
“Mradi huo ni mkubwa sana unaoshirikisha kampuni hii ya China Merchants Group, wawekezaji kutoka Oman ambao wataalamu wao pia wameshafika na Serikali ya Tanzania. Tunatarajia kuwa utaibadilisha Bagamoyo kwa kiasi kikubwa na kuufannya kuwa mji wa viwanda, hatua itakayovuta wawekezaji wengi zaidi na kuzalisha ajira nyingi,” alisema.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)