Msanii wa Coke Studio apongezwa kwa kushinda tuzo - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Msanii wa Coke Studio apongezwa kwa kushinda tuzo

Msanii aliyeshiriki katika msimu wa tatu wa Coke Studio unaoendelea kuoneshwa Clouds TV Vanessa Mdee, amepongezwa kwa kupata tuzo ya msanii bora wa kike Afrika Mashariki kwenye tuzo za Afrimma zilizofanyika Marekani hivi karibuni.

Pongezi hizo zimetolewa na kampuni ya Coca-Cola ambayo inaendesha onyesho la kusisimua ya muziki la Coke Studio ambalo linaendelea nchini kupitia luninga ya Clouds na kuwavutia watazamaji wengi wa muziki nchini ikiwemo nchi nyingine za Africa.

Meneja wa Biashara za Coca-Cola nchini, Maurice Njowoka amesema kuwa wanajivunia kuona mshiriki wa Coke Studio mwaka huu anazidi kupata mafanikio kwa kushinda tuzo nyingine zaidi.

“Mafanikio ya Vanessa yametufurahisha sana akiwa ni mmoja wa wasanii wa Coke Studio mwaka huu tuna imani naye kubwa kuwa ataendeleza kipaji chake cha muziki na kuweza kupata mafanikio zaidi”
Wasanii wanne kutoka Tanzania waliopo kwenye msimu wa tatu wa Coke Studio mwaka huu  ni Ben Pol ambaye alifanya kolabo matata(mash-up) pamoja na  mwanamuziki nguli kutoka Kenya anayejulikana kama Wangechi, Fid Q amefanya bonge la kolabo (mash-up) na Maurice Kirya kutokana Uganda, Gwiji wa Bongo fleva nchini Ali Kiba amefanya kolabo matata(mash-up) na Victoria Kimani kutoka nchini Kenya na wakati Vanessa Mdee amefanya kolabo matata(mash-up) na  mwanamuziki nguli kutoka nchini Nigeria ajulikanaye kama 2Face.

Wanamuziki wengine wa Tanzania  walioshinda tuzo za Afrimma ni Diamond Platnumz ambaye alifanikiwa kukomba tuzo 3 ambazo ni Video bora ya kucheza NANA, Msanii bora wa Afrika Mashariki na msanii wa mwaka, Diamond pia alishiriki kwenye msimu wa pili wa Coke Studio mwaka jana.
 
Ommy Dimpoz naye alijishindia tuzo ya msanii bora anayechipukia.

 About The Coca-Cola Company:
The Coca-Cola Company (NYSE: KO) is the world's largest beverage company, refreshing consumers with more than 500 sparkling and still brands. Led by Coca-Cola, one of the world's most valuable and recognizable brands, our Company's portfolio features 20 billion-dollar brands including Diet Coke, Fanta, Sprite, Coca-Cola Zero, vitamin water, Powerade, Minute Maid, Simply, Georgia and Del Valle. Globally, we are the No. 1 provider of sparkling beverages, ready-to-drink coffees, and juices and juice drinks. Through the world's largest beverage distribution system, consumers in more than 200 countries enjoy our beverages at a rate of 1.9 billion servings a day. With an enduring commitment to building sustainable communities, our Company is focused on initiatives that reduce our environmental footprint, support active, healthy living, create a safe, inclusive work environment for our associates, and enhance the economic development of the communities where we operate. Together with our bottling partners, we rank among the world's top 10 private employers with more than 700,000 system associates. For more information, visit Coca-Cola Journey at www.coca-colacompany.com, follow us on Twitter at twitter.com/CocaColaCo, visit our blog, Coca-Cola Unbottled, at www.coca-colablog.com or find us on LinkedIn at www.linkedin.com/company/the-coca-cola-company.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages