Picha Kwa Hisani ya Mtandao
Yakiwa yamebaki masaa takribani 29 kwaajili ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini Tanzania ambao watanzania tunakwenda kuchagua Rais wa Awamu ya Tano, wabunge na Madiwani basi tunatakiwa kufahamu au kupata elimu kidogo ya Zoezi hili linalofanyika kila baada ya Miaka Mitano kwa Nchi yetu ya Tanzania. Basi hapa chini Ni elimu juu ya siku hiyo unachotakiwa kufanya katika chumba cha Kupigia Kura.
Unapoenda Kupiga kura siku ya tarehe 25 Oct Msimamizi wa Uchaguzi atakapokupa karatasi ya kupigia kura hakikisha una weka tiki ndani ya sanduku la Mgombea Umpendae au unayeona Unastahili kumchagua wewe na tiki hiyo iwe ndani ya kisanduku hiko na Sio itokeze hadi nje ya kisanduku hiko
Vilevile endapo kuna mgombea humpendi/Hutaki kumchagua usihangaike nae hata kidogo unachotakiwa kufanya ni kuweka tiki tu kwenye kisanduku cha umtakaye wewe awe kiongozi wako.
Kuweka alama kwenye sehemu ya mgombe usiyemtaka, kuweka alama yoyote ile kwenye picha ya mgombea usiyemtaka, Kuweka alama ya X kwenye kisanduku cha mgombea usiyemtaka na kumchora kwenye kisanduku cha mgombea usiyemtaka hapo utakuwa umeharibu Kura yako na Mgombea Umtakaye atakuwa amekosa Kura yako hiyo Muhimu.
Usipaniki wala Kuwa na Jazba kwenye Chumba cha kupigia Kura Kwasababu sio ugomvi wala Kuvunja sheria Nenda kapige kura uchague kiongozi unayehisi atakuletea maendeleo
Niwatakie Uchaguzi Mwema Watanzania wenzetu na tujitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura Kubaki Kushabikia Nampenda huyu simpendi yule hakutasaidia kama hutopiga kura. Mapenzi yako kwa Mgombea wako ukayaonyeshe kwenye Sanduku la Kupigia kura kwa kumchagua
Lukaza Blog tunaamini kuwa hakutakuwa na vurugu wala Vurumai Naamini Zoezi hili litafanyika kwa Uweledi wa Hali ya Juu na Kwa Amani Kabisa.
Mungu Ibariki Tanzania





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)