Pages

DK MAGUFULI ASHIRIKI KUUPOKEA MWILI WA MAREHEMU DK KIGODA DAR

 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akizungumza na vyombo vya habari jinsi alivyomfahamu aliyekuwa waziri wa Viwanda na Biashara, marehemu Dk Abdallah Kigoda wakati wa mapokezi ya mwili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dcar es Salaam jioni hii, ukitokea India ambako alipatwa na mauti.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, na Mgombea ubunge Jimbo la Handeni kupitia CCM, marahemu Dk Abdallah Kigoda, ukihamishiwa kwenye gari lingine wakati wa mapokezi ya mwili huo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam jana, ukitokea nchini India ambako alipatwa na mauti. Mwili huo ulikwenda kuhifadhiwa Hospitali ya Jeshi ya Lugalo, kusubiri kuagwa leo katika Ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam



 Dk Magufuli akimfariji mtoto wa marehemu Dk Kigoda kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam

 Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha Rose Migiro akimfariji dadake na marehemu Dk Kigoda, Dk Aisha Kigoda..PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

 Mkuu wa Mkowa wa Tanga, Mwantumu Mahiza akimfariji mjane wa marehemu Dk Kigoda, Rasul Kigoda

 Dk Magufuli akizungumza jambo na Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue wakati wa mapokezi ya mwili wa marehemu Dk Kigoda Uwanja wa Ndege.

 Dk Magufuli akisalimiana na wananchi waliofika kuupokea mwili wa marehemu Dk Kigoda

Dk Magufuli (kulia) akiangalia jeneza lenye mwili wa Dk Kigoda ukishushwa wakati wa mapokezi ya mwili huo kwenye Uwanja wa Ndege, Dar..PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)