CHADEMA MONDULI WASEMA WAO WATAANZA NA ELIMU - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

CHADEMA MONDULI WASEMA WAO WATAANZA NA ELIMU


Mgombea udiwani monduli mjini kwa Tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Izak Joseph akihutubia mamia ya wakazi wa mji wa Monduli juzi katika viwanja vya  soko la alhamis  wakati akizindua rasmi kampeni za mgombea huyo.
************

Wagombea Udiwani na Ubunge jimbo la Monduli kupitia Chama  cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wametaja sekta ya elimu kuwa moja ya vipaumbele watakapofanikiwa kushinda uchaguzi mkuu ujao.


Akihutubia mkutano wa kampeni mjini Monduli juzi, mgombea ubunge kupitia Chadema Julius Kalanga alisema elimu ni msingi wa maendeleo katika sekta zote kwa sababu ndio huzalisha wataalam na watendaji katika miradi yote ya maendeleo.


"Aliyekuwa mbunge wa Monduli, Mheshimiwa Edward Lowassa  amefanya makubwa katika sekta ya elimu, siyo tu Monduli, bali eneo lote  la jamii ya wafugaji wa Kimaasai ambao kihistoria walionekana kubaki nyuma kieleimu. Nitaendeleza yote," alisema Kalanga


Alitaja vipaumbele vingine kuwa ni afya, miundombinu, mawasiliano, uwezeshaji na uimarishaji wa miradi midogo midogo kupitia  vikundi vya ujasiriamali pamoja na uhamasiahaji wa umma kushiriki harakati za maendeleo kwa kupanga, kuchangia, kitekeleza na kusimamia miradi katika maeneo yao.


Kwa upande wake, mgombea udiwani kata ya Monduli mjini, 
Isack Joseph "Kadogoo" anayetetea nafasi yake aliahidi kuendelea 
kuwalipia ada wanafunzi wote watakaofauli kuendelea na elimu ya 
sekondari ndani yakata yake, lakini wazazi au walezi hawana uwezo wa 
kugharamia elimu yao.


"Tangu niwe diwani mwaka 2010 hadi sasa nimeshawalipia 
zaidi ya wanafunzi 75 wanaosoma shule mbalimbali za sekondari ndani na 
nje ya wilaya ya Monduli. Nitaendelea kufanya hivyo," alisema Joseph


Alisema awali alikuwa akitumia fedha zake binafsi kabla ya 
kuingiza programu hiyo katika mipango ya matumizi ya fedha za maendeleo 
ya kata ili kuwezesha mradi wa ada kwa wanafunzi kuwa endelevu kwa kila 
diwani atakayefuata badala ya kubaki jambo lake binafsi.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages