Pages

ABDULMALIKI MOLLEL: WANAFUNZI WANAOSOMA NJE YA NCHI WANA UWIGO MKUBWA WA KUAJIRIKA


Na Mwandishi Wetu, Arusha.

VITU vinavyofanya wanafunzi kwenda kusoma nje ya nchi ni kutokana kozi wanayoenda kusoma zina uwigo mkubwa wa ajira ambapo vyuo vya ndani havina kozi hizo.

Akizungumza na katika kongamano la saba la vyuo vikuu la kujadili mstakabali wa elimu nchini, lililofanyika jijini Arusha mwishoni mwa wiki iliyopita, Mkurugenzi wa Global Link Education (GEL), Abdulmaliki Mollel amesema kuwa wanafunzi kwenda nje inatokana na kuangalia fursa za kusoma huko ambazo nchini hazipatikani nchini.

Amesema kuwa changamoto nyingine inatokana na masomo waliochagua kutokana na uchaguzi mdogo kutokana na vyuo inawafanya wanafunzi watafute vyuo vya nje ili waweze kusoma na kuwa na uhakika wa ajira.

Mollel amesema katika mazingira ya sasa teknolojia ya kufundisha wanafunzi ni finyu ukilinaganisha na vyuo vya nje kutokana na uwekezaji katika elimu ambayo hauwezi kuwa sawa na uwekezaji wa vyuo vya ndani.

Aidha amesema kuwa ufundishaji wa wanafunzi wa vyuo vya nje unatofautiana hivyo wazazi kuwa na ushawishi wa kuwekeza elimu kwa watoto wao kutokana na vyuo vya nje vimewekeza kwa wahadhiri kwa wanafunzi wanne Profesa mmoja.

Mollel amesema kuwa kuna kozi zilizopo nchini zinafanya watu wasiweze kuajirika kutokana na mabadiliko ya elimu zimebaki pale pale bila kuongezea vitu mbadala ambayo ni tofauti na vyuo vya nje vimweza katika fani zilizopo nchini hazina ajira wameongeza vitu na kufanya watu watake kusoma vyuo vya nje

“Maisha yanabadilika mwanafunzi akisoma ndani na kuona aliyesoma nje ana uwigo wa ajira inawafanya kuwashauri wazazi wao kwa waliobaki wasome nje ili waweze kuona mafanikio ya ajira yake” amesema Mollel.

Ameongeza kuwa kutokana na vyuo kuwa na kozi mbalimbali ambazo kwa sasa haziwezi kutoa fursa GEL inaweza kuunganisha na vyuo vya nje kuweza kuingiza mtaala katika vyuo vya ndani kwa kuingia mikataba ambayo itasaidia vijana wanaohitimu kuwa na uwigo ajira na uwezo wa kujiajiri.

Mollel amesema GEL imeweka mazingira rafiki kwa wanafunzi wanaosoma nje kwa kufanya ufatiliaji juu ya maendeleo yao na wanavyorudi wamekuwa na uwigo wa kuajirika na kufanya wachague kazi kutokana na maarifa walioyapata nje.

Mkutano wa kujadili mstakabali wa elimu nchini uliyoandaliwa na wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kushirikiana naTume ya Vyuo Vikuu nchini, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) pamoja na Kamati ya Wakuu wa vyuo Vikuu nchini (CVCPT) ulionza na Oktoba 1 na kumalizaka oktoba 2 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)