Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa(Tanapa)Allan Kijazi akiwa kwenye mazungumzo na Balozi wa Uturuki nchini, Yasemin Eralp(katikati)aliyefika makao makuu ya Shirika hilo leo,kulia ni Katibu Msaidizi wa Ubalozi wa Uturuki,Berat Colak. |
Balozi wa Uturuki nchini, Yasemin Eralp(kushoto) akipokea zawadi
kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Tanapa,Allan Kijazi alipotembelea Makao Makuu ya shirika hilo jijini Arusha. |
Balozi
wa Uturuki nchini Mhe. Yasemine Eralp amesema atawaalika wawekezaji kutoka
Uturuki ili waweze kutumia fursa za uwekezaji zilizopo katika Hifadhi za Taifa
nchini. Balozi Eralp alitoa ahadi hiyo alipotembelea Makao Makuu ya TANAPA
jijini Arusha na kukutana na viongozi wa shirika.
Balozi
Eralp amesema kuwa sekta ya utalii ni miongoni mwa vipaumbele vyake na kwamba
atatumia muda wake mwingi kuhakikisha kuwa sekta hiyo inastawi na kuvutia
watalii wengi nchini kutoka Uturuki.
Katika
mazungumzo yake na viongozi wa TANAPA, Balozi Eralp alitoa nafasi kwa TANAPA
kutangaza katika Jarida la Shirika la Ndege la Uturuki Skyline Magazine,
na
kwamba fursa hii itasaidia kuvutia wageni wengi zaidi nchini kutoka nchi
zaidi ya 60 zinazofikiwa na shirika hilo la ndege ulimwenguni.
Balozi
Eralp alikubaliana na TANAPA kuwa atafanya mazungumzo na Turkish Airline ili
waweze kuandaa safari za kutembelea vivutio vya utalii katika hifadhi kwa
waandishi wa habari na mawakala wa wageni kutoka Uturuki ili waweze kuzitangaza
Hifadhi za Taifa katika Bara la Ulaya.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi aliahidi kuwa TANAPA itatoa
ushirikiano wa dhati katika kuhakikisha kuwa malengo ya Mhe. Balozi Eralp
yanatimizwa ikiwa ni pamoja na shirika
kutumia fursa ya kupata watalii kutoka Uturuki ambayo ni miongoni mwa nchi
ambazo uchumi wake unakua kwa kasi kubwa na kuwa fursa za kupata wageni wengi
zaidi kutoka Uturuki zinaonekana
dhahiri.
Imetolewa
na Idara ya Mawasiliano
na Idara ya Mawasiliano
Hifadhi
za Taifa Tanzania
za Taifa Tanzania
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)