Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro (PICHA MAKTABA) |
Na Kahema Emanuel,Mbeya
Wito umetolewa kwa Waratibu wa uchaguzi wa mikoa ,wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi pamoja na maafisa uchaguzi wa halmashauri mikoa ya kanda za juu kusini kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa waledi na kwa uadilifu bila kuwa na upendeleo wa chama chochote cha siasa ua mgombea .
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro wakati akifungua mafunzo ya wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi pamoja na maafisa uchaguzi halmashauri ambao ni wakurugenzi wa halmashauri na maafisa uchaguzi katika mikoa ya Iringa na Mbeya.
Amesema ili zoezi hilo la uchaguzi liende vizuri na lisighubikwe na vurugu nivema
wasimamizi hao wakatumia waledi wao na udilifu bila kuwa na upendeleo wa chama chochote cha siasa au mgombea yoyote ili kuepuka hali hiyo.
Amesema mara baada ya kupatiwa mafunzo hayo nivema wakaendelea kutumia muda wao wa ziada kusoma na kupitia vitabu vya maelekezo waliyopatiwa kwa kutumia kanuni na maadili ya uchaguzi ili kuimarisha uelewa zaidi kuhusu wajibu na majukumu yao katika zoezi hili la uchaguzi mkuu mwezi octobar.
Amesema pamoja na majukumu mengine waliyonayo pia wametakiwa kutoa kipaumbele katika kutekeleza zoezi hili la kitaifa kwa ufanisi zaidi na kwa muda uliopangwa kwani
uchaguzi huu utafanyika kwa siku moja tu kwa kila baada ya miaka mitano.
Aidha amesema kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetekeleza jukumu lake katika hatua ya
mafunzo na maandalizi ya vifaa na rasilimali nyingine hivyo wao kama wasimamizi wanatakiwa kutekeleza wajibu wao katika ngazi zote kwa mujibu wa taratibu zilizopangwa na Tume.
Katika semina hiyo wasimamizi hao watajifunza wajibu wa wasimamizi wa vituo vya kupigia kura ,uwendeshaji wa zoezi la upigaji kura vituoni sanjali na uendeshaji wa zoezi la kuhesabu kura,kujumlisha kura na kutanganza matokeo ya uchaguzi.
Afisa Uchaguzi Kanda ya Nyanda za juu kusini -Tume Ndugu Jane Tungu akizungumza katika semina hiyo. |
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)