Shinyanga Rural Farmers’ representatives together with Agrics team during the workshop for contract signing which was held at Ishololo village in Shinyanga Rural district. The workshop lead by Mr. Lazaro Japhet (standing-third from left, front line) is the preparation of farm inputs distribution for the coming farming season in September 2015 where more than 12000 farmers expect to benefit with cetcfied seeds of maize and sunflower from Agrics company
Agrics Maize seed germination tests with success of 100% outcome to prove the viability of their seeds. These are among certified seeds which are going to be distributed to farmers in Northern Tanzania (Shinyanga and Simiyu regions) as 12,000 farmers expect to benefit them from Agrics company’s as now farmers prepare to start new farming season.
Mahindi yaliyooteshwa kisayansi na kampuni ya Agrics kwa lengo la kuthibitisha ubora wa mbegu zinazotolewa kwa wakulima wa kanda ya ziwa. Zaidi ya wakulima 12000 watanufaika na mbegu izo msimu huu. Matokeo ya vipimo yalisadifu ubora wa kampuni ya Agrics kwa kutoa asilimia 100% ya ubora.
Kufuatia msimu mpya wa kilimo unaotarajia kuanza hivi karibuni. Kampuni ya Agrics inatarajia
kuwanufaisha wakulima 12,000 wa Shinyanga vijijini, Maswa na Meatu kwa kuwapatia mbegu
bora za mahindi, alizeti pamoja na mbolea ili kuhakikisha kilimo biashara kinainuliwa na kuleta
tija kwa mkulima. Mbegu hizo zitatolewa hivi karibuni ili kuhakikisha mkulima anakuwa na
maandalizi ya uhakika msimu huu. Kampuni ya Agrics hutoa mbegu kwa mkopo nafuu
unaolenga kumnufaisha mkulima kwa mazao mengi zaidi. Pia Agrics ikishirikiana na viongozi wa
serikali huwanufaisha wakulima kwa kuwapatia mafunzo katika ngazi tofauti za ukuaji wa
mazao ili kuhakikisha mavuno yanasadifu malengo ya wakulima hao.
Akiongea kwa niaba ya kampuni ya Agrics, Meneja Miradi Bw. Charles Laswai alithibitisha ubora
wa mradi huo wakati akikabidhi mikataba ya uchaguzi wa mbegu kwa wakulima. ‘’ Ni miaka
mitano sasa tangu Agrics ianze kutoa mbegu bora kwa mkopo kwa wakulima wetu wa kanda ya
ziwa. Kwa sasa wakulima wameelewa zaidi umuhimu wa kilimo biashara. Mkulima anavuna
zaidi ya asilimia arobaini kulinganisha na kabla ya kujiunga na mradi huu wa kukopeshwa
mbegu na mbolea kwa ajili ya kilimo bora. Na kwa mwaka huu tunategemea mavuno mazuri
zaidi kwani hali ya hewa itakuwa nzuri kutokana na vyanzo vya taarifa ya hali ya hewa nchini’’.
Wakulima wamekuwa wakikutana na changamoto mbalimbali zikiwemo ukosefu wa mikopo
kwa ajili ya kilimo na ukosefu wa elimu juu ya kilimo bora chenye tija. Agrics ikiwa kama chachu
ya mabadiliko kwa mkulima wa kanda ya ziwa, imekuwa ikiwakopesha mbegu na mbolea
zilizothibitishwa kwa ubora, mkulima hutoa asilimia kumi wakati wa kuomba aina ya mbegu
aitakayo na badae hutoa asilimia 15 wakati wa kukabidhiwa mbegu husika. Mkulima hupewa
nafasi ya kuwa huru na kusimamia kilimo chake huku akiendelea kupata mafunzo na ushauri
kutoka kwa afisa miradi wa Agrics ili kuhakikisha malengo ya mkulima yanatimia na anazalisha
kwa kiasi kikubwa. Mkulima humalizia asilimia 75% ya deni lake kwa awamu tatu zinazompa
muda wa kutosha baada ya kuwa amevuna.
“Ni kampuni ya Agrics iliyoyabadilisha maisha yangu kufikia mafanikio haya niliyonayo. Kiujumla
wamebadilisha maisha ya wakulima wa hapa kijijini na kutufanya tuuage umasikini. Nilikuwa
nikivuna gunia nne katika hekari moja lakini kwa sasa navuna zaidi ya gunia kumi kulingana na
muitikio wa mvua. Tangu kujiunga na Agrics nimewapeleka watoto watatu sekondari na
ninamiliki pikipiki kutokana na mavuno yangu. Sijawahi kuishiwa chakula kwani huwa ninaweka
SIMIYU NA SHINYANGA.
akiba ya kutosha kwa ajili ya familia yangu’’. Alieleza Bw. Steven Kanogu mkazi wa kijiji cha
Ishinabulandi wilaya ya Shinyanga vijijini wakati akipokea mkabataba wa mkopo wa mbegu na
mbolea kwa ajili ya kilimo cha msimu huu.
Agrics Ltd ni kampuni ya kibiashara inayofanya kazi zake kwa kushirikiana na shirika la ICS.
Agrics inawapa wakulima wadogo wa kanda ya ziwa nchini Tanzania na Kenya fursa ya kujipatia
mbegu bora na za kisasa kwa mkopo nafuu unaolipwa kwa awamu zinazompa mkulima nafasi
nzuri ya kujiendeleza. Pia Agrics inahakikisha akiba ya chakula kwa mkulima ni lazima kwa ajili
ya kupunguza njaa kwa wakulima. Kwa mawasiliano Zaidi tembelea tovuti yetu www.agrics.org
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)