UFAHAMU VYEMA MOYO WAKO "CARDIAC ARRHYTHMIA" - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

UFAHAMU VYEMA MOYO WAKO "CARDIAC ARRHYTHMIA"

‘Cardiac Arrhythmia’ ni pale mtu anapokuwa na mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida au yanayodunda sana. Mwili una mfumo asili wa umeme unaosaidia  moyo kufanya kazi. Mfumo huu husababisha moyo kutanuka na kusinyaa  ambapo husababisha damu kuingia na kutoka kwenye moyo; umeme kwa kawaida hufuata mkondo na mapigo ya moyo kwa kasi ya kawaida. Ingawa, kama  mkondo wa kawaida wa umeme huu ukivurugwa moyo hushindwa kufanya kazi na kusababisha mapigo ya moyo ama kwenda taratibu sana, haraka sana au  yasiyoimara.


Kuna aina kadhaa za ‘Arrhythmia’; Baadhi ni pamoja na zijulikanazo kitaalamu kama Supra-Ventricular Tachycardia, Ventricular Tachycardia,  Ventricular Fibrillation, Atrial flutter and Atrial Fibrillation. Mapigo ya moyo yasiyo imara hasa husababishwa na ugonjwa wa moyo na moyo   kushindwa kufanya kazi. ‘Arrhythmia’ ndogo pia huweza kusababishwa na  mtindo wa maisha usiozingatia afya bora ikiwa ni pamoja na uvutaji  sigara uliopitiliza, Ulevi na kuzidisha matumizi ya kafeini au msongo wa mawazo.


Ingawa imegundulika hasa katika uchunguzi wa mara kwa mara wa matibabu dalili  za ‘arrhythmia’ ni chache zinazoweza kuonekana ikiwa ni pamoja na 


 kuongezeka kwa mapigo ya moyo, kupungua kwa mapigo ya moyo, maumivu ya  kifua, kizunguzungu, kuchoka sana na kukosa pumzi.

‘Arrhythmia’ mara nyingi hutokea kwa nyakati tofauti tofauti. Hali ya kutotabiri kwa ‘arrhythmia’ na kutokea kwake kwa nyakati tofauti tofauti hufanya uchunguzi kuwa mgumu. Moja ya vifaa vitumikavyo zaidi kwa uchunguzi wake kitaalamu ni ‘electrophysiology (EP)’ na kinachukuliwa kuwa bora zaidi  katika taaluma hii.


Utafiti wa EP hufanya kazi kwa kupima na kurekodi shughuli za umeme wa moyo na  kuonesha njia za umeme. Inaonesha sababu na mahala penye tatizo la 


mapigo ya moyo. Matatizo yanayotokea katika utafiti wa EP ni machache 
sana kwa kuwa umekuwa ukifanyika salama kwa miaka mingi sasa.

Taarifa inaweza kuundwa katika namna mbili, ama kupitia ramani ya shughuli za  umeme wa moyo kupitia kifaa maalumu kitaalamu ‘electrocardiogram (ECG)’ 


 inayoonesha wapi ishara zisiyo za kawaida zinaanza kutokea ndani ya 
moyo.


Mfumo wa wa kitaalamu wa ‘Carto3’ ujulikanao kama ‘3D mapping’ ni teknolojia  mpya inayotoa muonekano wa moyo kwa ukubwa mara tatu zaidi. Hii 


 hupelekea kuboreshwa kwa usahihi wa vipimo na matibabu ya mgonjwa.

Kwa kesi ya kushuka kwa mapigo ya moyo, utafiti wa EP unatoa nafasi 
kutathmini haja ya vifaa kama vile ‘peacemaker’ au ‘defibrillator’   ambavyo husaidia kuzuia vifo vya ghafla vya magonjwa ya moyo.


Baada ya uchunguzi kupitia utafiti wa EP, mirija maalum ya ‘Radiofrequency   (RF) catheter ablation’ huingizwa katika mishipa ya damu ambapo viwango  vya juu na vya chini vya mzunguko wa nguvu ya umeme vinapokelewa katika  tishu za moyo na kuharibu tishu zile zinazohusika na mapigo ya moyo  ‘arrhythmia’. Baada ya matibabu kwa kawaida wagonjwa sasa huweza  kikamilifu kupunguza matumizi ya dawa ambapo mgonjwa ataweza kupumua  vizuri na mapigo ya moyo kwenda vizuri. 


kwa mujibu wa Dkt A M Karthigesan wa hospitali za Apollo baadhi ya arrthythmia’ zilitibiwa kupitia kipimo maalumu kijulikanacho kitaalamu 


 kama ‘RF Ablation’ ni ‘Supraventrical Tachycardia (SVT’; hii inatokea 
kwenye vyumba vya juu vya moyo na kwa ujumla inaelezewa kama moyo kupiga kwa kasi. Pingili za ‘Atirioventrikali (AVNRT)’, ‘atirioventrikali 


reentry (AVRT)’ na ‘focal atrial tachycardia’ ni baadhi ya aina nyingi  za SVT. 



Zaidi ‘Atrial Flutter (AFL)’ inaweza pia kutibiwa kwa upasuaji wa RF. AFL ni 

wakati atria inapopiga haraka sana kwa kiwango cha karibu mapigo 300 kwa  dakika yanayotokea katika chumba cha juu cha moyo. Arrhythmia

nyingine maarufu inayotibiwa kwa RF ni ‘Atrial Fibrillation (AF)’. Hii 
ni wakati uwezo wa moyo kufanya kazi zake unapunguzwa kwa mapigo yasiyo  na mpangilio ya chumba cha juu cha moyo. Ingawa ‘atrial fibrillation’  haitishii maisha, kuongezeka kwa mapigo ya moyo huweza kupelekea   matatizo kama vile damu kuganda ambapo hatimaye inaweza kusababisha  kiharusi.


‘Ventricular Tachycardia (VT)’ ambayo kama ikiachwa bila kutibiwa 
inaweza kuwa aina ya ‘Arrhythmia’ ya kuhatarisha maisha, hii hutokea 
wakati chumba cha chini cha moyo kikimpiga kwa kasi sana Dkt. A M Karthigesan wa hospitali za Apollo anasema kuwa baadhi ya manufaa  ya kufanyiwa tiba ya upasuaji kwa mirija ni kuwa mtu atarajie mabadiliko  ya haraka katika ubora wa maisha sababu ya kuongezeka kwa uwezo wake wa kufanya kazi; Huduma ya matibabu iliyoboreshwa kwa jinsi mgonjwa 

anavyohitaji imeondoa upotevu wa muda; Kupungua kwa gharama za tiba na  kuokoa maisha ambapo mgonjwa anapewa nafasi nyingine ya kuishi.

Imechangiwa na:
Dkt A M Karthigesan
Mshauri wa tiba ya umeme wa moyo
Hospitali za Apollo, Chennai

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages