UBORESHAJI WA USALAMA BARABARANI KWA USAFIRISHAJI WA MASAFA MAREFU. - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

UBORESHAJI WA USALAMA BARABARANI KWA USAFIRISHAJI WA MASAFA MAREFU.


 Fuso ikipita Njiani kwenye Maonyesho ya "NDIO Fuso ni Faida" jijini Dar, Maonyesho hayo yanatarijiwa kupita kwenye Mikoa kama Tanga – Moshi- Arusha- Mwanza –Shinyanga -Kahama- Dodoma – Iringa – Mbeya  na Songea ambapo shughuli mbali mbali za uchimbaji wa 
madini, kilimo, ujenzi na usafirishaji wa mizigo zinafanyika
 Wadau wa Usafirashaji wakiwa katika Maonyesho ya 'Fuso ni faida' jijini Dar
 Wadau wakipata maelekezo ya Huduma ya 'Ndiyo Fuso ni Faida'
Na Mwandishi Wetu,

Mtandao wa miundombinu ya barabara nchini Tanzania inayokadiriwa kuwa na kilometa za mraba 91,049 ambayo ni mara 30 zaidi ya mtandao wa reli ambayo inaambaa kwenye eneo lenye ukubwa wa takribani kilomita za mraba 3,682 ikidhihirisha kuwa barabara ndiyo njia kuu inayopendelewa kutumika katika usafirishaji wa mizigo.

Usafirishaji nchini Tanzania unajumuisha mitandao ya barabara, anga, reli na maji ambapo katika njia zote hizi, barabara na reli zinaongoza zikifuatiwa na maji na anga.  Hakika katika suala la umbali, mtandao wa barabara za Tanzania unashika nafasi ya 51 duniani, kutokana na taarifa zilizonukuliwa katika kitabu “ CIA world fact book” Wakati ajali za barabarani zikiendelea kugharimu maisha ya watu, ufanisi wa  njia hii ya usafirishaji kwa ujumla wake unahitaji kudumisha ubora wa 

usafirishaji wa barabara nchini Tanzania kutokana na ufanisi wake, 
kuokoa mda na kuaminika pamoja na kuchukuliwa kuwa kiunganishi kikubwa  cha barabara ndogo kwenye barabara kuu za nchi.


Diamond Motors limited hivi karibuni wamekuwa katika safari ya kuzunguka  mtandao huu wa barabara wakihamasisha pamoja na mambo mengine usalama 


 barabarani katika kampeni yao ya “Ndio! Fuso ni Faida” Kampeni hiyo 
iliyozinduliwa mwezi julai mwaka huu jijini Dar es salaam ilifika katika
mikoa ya Tanga-Moshi- Arusha – Mwanza – Shinyanga – Kahama – Dodoma – 
Iringa – Mbeya – na Songea ambapo shughuli mbali mbali za uchimbaji wa 
madini, kilimo, ujenzi na usafirishaji wa mizigo zinafanyika. Pamoja na 
mambo mengine, kampeni hiyo ilidhamiria kujenga uelewa kwa wateja wake  juu ya jinsi ya kuboresha usafirishaji salama wa mizigo kwa kutumia 


 magari ya kisasa zaidi.


Akifafanua kwa undani juu ya malori mapya yaliyohusika katika kampeni hiyo ya  “Ndio! Fuso ni Faida” msemaji rasmi wa kampuni ya Diamond Motors Limited


 ambao ni wadau na wataalamu katika sekta ya usafirishaji wa masafa 
marefu kwa kutumia malori yao ya Fuso alisema soko la Tanzania 
linahakikishiwa malori ya aina ya Fuso FZ na FJ yaliyoboreshwa 
kiteknolojia na kuwa na uwezo wa kuboresha usalama barabarani.  “Malori 
haya yametengenezwa na kitako imara kilichotengenezwa kwaajili ya uzito 
mkubwa na mazingira magumu ya kufanya kazi” alisema Meneje Mkuu (Masoko) wa diamond Motors Ltd bwana Laurian Martin.  Aliongeza kusema kuwa  “tuna nia ya kuborsha sekta ya usafirishaji iliyo bora na salama kwa 


kutumia malori yetu ya Fuso yaliyo boreshwa ki teknolojia”

Alisistiza na kusema kuwa “aina mbali mbali mpya za malori yatolewayo na Diamond  Motors Ltd sio yanaaminiki katika utendaji tu, bali pia yana uwezo 


mkubwa wa ubebaji ambayo ni sifa pekee isiyopatikana katika malori 
mengine ambayo yanalazimika kutumia mafuta mengi ili kukidhi kigezo 
hicho. Kizuri zaidi, malori haya gharama zake za matengezo ni ndogo 
zaidi na hutembea umbali mrefu zaidi wa takribani kilomita 45,000 kabla 
ya kuhitaji matengenezo ya kawaida kama kubadilisha vilainishi”.


Bwana Laurian Martin aliendelea kusema kuwa “Sifa hizi ndizo zinafanya malori ya Fuso FZ na FJ kuwa suluhisho kamili la usafirishaji na biashara 


 nchini Tanzania”. Katika kampeni hiyo mikoa ya kaskazini ikiwemo Tanga, 
Kilimanjaro, na Arusha ilipata  fursa ya kuona faida zinazopatikana 
katika malori haya mbalimbali ya Fuso maboyo ni malori ya ubebaji mkubwa yanayopatikana katika kampuni ya Diamond Motors Ltd.  Miji ya mikoa hii imendelea kukua katika shughuli za kiuchumi kama vile usafirishaji wa mizigo, biashara, viwanda kama vile cementi, malighafi mbalimbali, maua,matunda, mazao mbalimbali yatokanayo na miti yanayohitaji kusafirishwa kwenda katika sehemu mbalimbali za nchi na nje ya nchi.  Wasafirishaji kutoka mikoa hii wameaswa kutumia teknolojia hii ya malori ya Fuso FZ na FJ ambayo inaweza kuwapatia Faida zaidi katika biashara zao.


Kampeni hiyo pia  ilifika katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha ambayo 
imeunganishwa katika ukanda wa kaskazini na barabara za nchi za jirani 
kama Kenya na Uganda kupitia mipaka yake ya Namanga ikiwa na biashara 
nyingi baina ya nchi hizo zinazopitia njia ya barabara.  Wakazi na 
wafanyabiashara waliohudhulia kampeni hiyo walipata fursa ya kujionea 
sifa zipatikanazo katika malori hayo ya Fuso Fz kutoka Diamond Motors 
Limted ambayo yanauwezo wa kubeba mizigo mikubwa katika mazingira magumu katika ukanda huo.  “Ni kwa teknolojia ya kisasa ya magari haya mabapo   wafanya biashara wanaweza kupata Faida ya biashaza zao kwa kutumia  malori haya inayotumia mafuta vizuri, ambapo gari hii ina kifaa maalumu cha kuzuia mafuta yasitumike endapo gari hii inatembea katika mteremko  ili kukupa umbali mrefu zaidi kwa mafuta kidogo. Mikoa ya Mwanza na Shinyanga ambayo ni kitovu cha biashara, usafirishaji, 

ushirikano wa kikanda na maendeleo ya kiuchumi katika kanda ya ziwa 
ikiunganishwa na bandari kavu ya Isaka, ilifikiwa na maonyesho haya ya 
Fuso Fz.  Mikoa hii pia inaunganisha nchi jirani za Uganda, Kenya, 
Rwanda, Burundi and Demokrasia ya Kongo ambazo ni nchi zenye biashara 
nyingi kubwa miongoni mwake na Tanzania.


Kwa usafirishaji wa masafa marefu katika nchi hizi, Fuso Fz ina muundo 
maridhawa kupasua upepo usiwe kizingiti ambayo haikupatii umbali mrefu 
tu, bali pia inampunguzia dereva uchuvu kwa kuwa na kibini 

iliyoninginizwa vizuri kupumguza sana mtikisiko wa barabarani hasa 

 kwenye matuta au barabara mbovu na kupunguza kelele za kutoka kwenye 
injini.  Sifa hii ni muhimu sana kumpunguzia dereva uchovu na hivyo 
kuweza kutosababisha ajali zitokanazo na uchvu wa dereva na kusinzia 
wakati akiendesha. 


Mikoa ya nyanda za juu kusini pia ilikuwa katika mpango wa kupata faida 
zitokanazo na matumizi ya malori mapya Fuso Fz yenye teknolojia mpya 
kutoka Diamond Motors ltd baada ya kufikiwa na kampeni hiyo ya “Ndio! 
Fuso ni Faida” Kampeni hiyo ilipokelewa vizuri na wakazi wa mikoa ya 
Dodoma, Iringa, Mbeya na Songea ambapo pia kuna shughuli za kiuchumi 
kama uchimbaji wa madini, kilimo cha chai, misitu na kilimo cha 
kibiashara.  Wafanyabiashara walionyeshwa haja ya wao kubadilisha njia 
za usafirishaji kwa kutumia Fuso Fz na Fuso FJ na hivyo kupunguza 
gharama za uendeshaji na kupata Faida zaidi katika biashara za kiuchumi 
nchini na ukanda wa Africa Mashariki na kati.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages