Tanzania imeisimamisha Malawi isiteketeze moto tani 2.6 ya pembe ya ndovu ilizonasa katika operesheni dhidi ya wawindaji haramu
Shehena hiyo ya meno 800 ya ndovu ilinaswa na maafisa wa forodha wa Malawi ilipokuwa ikiingizwa nchini Malawi.
Tanzania ilikimbia mahakamani ilikuizuia serikali ya Malawi isiharibu ushahidi wake dhidi ya watuhumiwa waliokamatwa na kesi inaendelea.
Mkurugenzi mkuu wa idara ya kuwalinda wanyama pori wa Malawi anasema kuwa inasikitisha mno kuwa Tanzania imekwenda mahakamani kuizuia idara yake isiteketeza bidhaa hizo haramu kwa miezi mitatu ijayo.
''Tulikuwa tayari kuchoma moto pembe hizo za ndovu ambayo ingekuwa ishara kamili kuwa tunapanga mikakati kabambe ya kupambana na walanguzi na wawindaji haramu ili kulinda ndovu wetu,''
''Sasa hilo halitawezekana kwa sasa na hadi baada ya miezi mitatu ijayo'' alifoka Bright Kumchedwa
Idadi ya ndovu imepungua kwa asilimia 50% tangu mwaka wa 1980 nchini Malawi kutokana na uwindaji haramu.
Nchini Tanzania Idadi ya ndovu imepungua kwa asilimia 60% katika kipindi cha miaka mitano tu iliyopita.
Mwezi uliopita mahakama moja iliwapata na hatia kaka wawili raia wa Malawi na hatia ya uwindaji haramu na ulanguzi wa pembe za ndovu.
Wawili hao walipigwa faini ya dola elfu tano za Marekani $5,500 na mahakama ikaamuru bidhaa hiyo ichomwe moto katika kipindi cha siku 20.
Lakini serikali ya Tanzania nayo ikakimbia mahakamani ilikuzuia serikali ya Malawi isiteketeza pembe hizo ikidai kuwa itakosa ushahidi wowote dhidi ya watuhumiwa wake wa uwindaji haramu.
Tatizo la uwindaji haramu umekithiri katika miaka ya hivi karibuni kufuatia utashi mkubwa wa bidhaa hiyo inayoenzia katika mataifa ya mashariki ya mbali na bara Asia.
Si aghalabu kushuhudia familia nzima ya ndovu na faru wakiangamizwa katika mbuga za wanyama pori barani Afrika ambako ndovu bado wapo.
Mwaka uliopita viongozi wa mataifa ya Botswana, Gabon, Chad na Tanzania yaliafikiana kuthibiti uuzaji wa pembe za ndovu. Chanzo bbc swahili
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)