Pages

MWILI WA BABA YAKE MWANAHABARI, PETER AMBILIKILE WAAGWA JIJINI DAR ES SALAAM, MAZISHI YAKE KUFANYIKA MBEYA LEO

 Marehemu Mzee Anyosisye Mwakyusa enzi za uhai wake.
 Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Anyosisye Mwakyusa, baba mzazi wa mwandishi mwandamizi wa gazeti la Jambo Leo, Peter Ambilikile, wakati wa ibada ya kumuombea iliyofanyika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Ubungo Kibangu Dar es Salaam jana, kabla ya kuusafirisha kwenda mkoani Mbeya kwa mazishi yatakayofanyika leo.
 Ndugu jamaa na marafiki wakiaga mwili wa marehemu.


 Waombolezaji wakiwa kwenye ibada ya kuuga mwili wa mzee wetu Anyosisye Mwakyusa.
 Familia ya marehemu ikiwa na huzuni wakati wa ibada hiyo.
 Waomblezaji wakiwa ibadani.
 Wafiwa wakipewa pole.
 Mwanahabari Peter Ambilikile aliyefiwa na baba yake 
akiwa katika huzuni.
 Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Ubungo Kibangu, Kishe Mhando (katikati), akiomba kabla ya kuanza kwa safari ya kwenda mkoani Mbeya.
 Mwili ukiondolewa kanisani.
 Waombolezaji wakisubiri gari lililobeba mwili huo kuondoka kwendaa mkoani Mbeya kwa mazishi.
Ni huzuni tupu.

Na Dotto Mwaibale

MZEE Anyosisye Mwakyusa ambaye ni baba wa Mwandishi Mwandamizi wa Gazeti la Jambo Leo, Peter Ambilikile mwili wake umeagwa jana kwenda mkoani Mbeya kwa maziko. 

Anyosisye alifariki juzi jijini Dar es Salaam kutokana na ugonjwa wa saratani uliokuwa ukimsumbua kwa muda mrefu.

Ibada ya kuaga mwili wa marehemu huyo ilifanyika  katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Ubungo Kibangu jijini  Dar es Salaam jana  ikiongozwa na Mchungaji Kishe Mhando wa ushirika huo.

Mchungaji Mhando alimwelezea Mwakyusa  kama mtu jasiri ambaye siku zote alikuwa mtu wa ibada na alikuwa akihudhuria ibada zote. Aliwaambia waumini kuwa mshahara wa dhambi ni mauti na mshahara wa kuwa na ibada ni maisha ya milele na Bwana Mungu. 

Alisema watu huwa wana ratiba yao na hakuna mtu hata mmoja anayejua ratiba ya Mungu. "Msiba hauchagui mtoto mchanga, mtu mzima, mwanamke au mwanaume. Mipango yote ni ya Mwenyezi Mungu, yeye ndiye anajua anayefuata ni nani," alisema.

Mazishi ya Mzee Mwakyusa yanatarajiwa kutafanyika mkoani nyumbani kwa marehemu eneo la Makungulu jijini Mbeya leo. Mwakyusa alizaliwa Mei 10, 1942. Alifunga ndoa yake mwaka 1968. Alifanya kazi serikalini na alistaafu mwaka 1980. 

Mwaka 1999  Mwakyusa alianza kulalamika kuwa na matatizo ya koo na kuanza kupatiwa matibabu katika hospitali mbalimbali, ikiwemo Hospitali ya Ocean Road hadi kifo chake. 

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)