Pages

MAANDALIZI YA TAMASHA LA KULIOMBEA TAIFA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU YA KAMILIKA LITAFANYIKA UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM, OKTOBA 4, 2015


 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Msama Promotion ambayo inaandaa matamasha mbalimbali kama lile la Pasaka  na Chrismas , ambaye ni Mwenyekiti wa Tamasha hilo, Alex Msama, akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya Tamasha la kuliombea Taifa Amani kuelekea uchaguzi mkuu ambalo litafanyika Oktoba 4, 2015 Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na baadaye mikoa mingine 12.
 Hapa mkutano na wanahabari ukiendelea.
Wanahabari wakisubiri kuchukua taarifa hiyo.


Na Dotto Mwaibale


Mwimbaji wa kimataifa wa nyimbo za injili kutoka nchini Afrika Kusini, Solly Mahlangu, amethibitisha 
kutumbuiza katika tamasha la kuombe amani  linalotarajiwa kufanyika Oktoba 4 katika uwanja wa Taifa 
jiji Dar es Salaam.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Msama Promotion ambayo inayoandaa matamasha mbalimbali kama lile la Pasaka  na Chrismas , ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tamasha hilo kutoka kampuni hiyo, Alex Msama wakati akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu kukamilika kwa  maandalizi ya tamasha hilo sambamba na kutaja majina ya waimbaji wa nyimbo za injili wa ndani na nje ya nchi, wanaotarajiwa kutumbuiza katika tamasha hilo linalolenga kuombea nchi amani  hususani uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba 25 mwaka huu.



''Maandalizi ya tamasha hilo yamekamilika na baadhi ya waimbaji wa nyimbo za injili tayari wamethibitisha kushiriki ambao ni  Solly Mahlangu, Kundi la Kelechi kutoka  nchini Uingereza nalo  pia limethibitisha kuja kutumbuiza katika tamasha hilo.''. alisema Msama. 

Msama amewataja Waimbaji wengine kutoka nje ya nchi ambao  wamekwisha kuthibitisha kuja kutoa burudani katika tamasha hilo  ni Sarah Kei na Solomoni Mukubwa kutoka nchini Kenya.

''Waimbaji wa ndani waliokwisha kuthibitisha kutumbuiza katika tamasha hilo la kuombea amani ni pamoja na Boniface Mwaitege,Rose Mhando,Upendo Nkone,Upendo Kilahiro, John Lissu,Christopher Mwangila,kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama na kwaya moja kutoka mkoani Iringa'', alisema  Msama.

Kwa mujibu wa Msama, tamasha hilo linalotarajiwa kuzunguka katika mikoa kumi na mbili ya Tanzania 
Bara, limelenga kuhubiri na kuiombea nchi amani,Upendo na mshikamano wakati na baada ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika kote nchini Oktoba 25 mwaka huu na kuiiniza madarakani serikali ya awamu ya tano. 



(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)