KUMBUKUMBU YA MIAKA 8 YA BABA MZAZI WA BLOGGER FATHER KIDEVU NA BIRTHDAY YA FATHER KIDEVU - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

KUMBUKUMBU YA MIAKA 8 YA BABA MZAZI WA BLOGGER FATHER KIDEVU NA BIRTHDAY YA FATHER KIDEVU

Mzee Shauri Timoth Nathan (18/08/1925 – 18/09/2007)
Mroki Mroki-Father Kidevu
Sekunde, Dakika, Saa, Siku, Wiki, Mwezi, Mwaka na hatimaye mika nane sasa imetimia tangu Mzee Shauri Timoth Nathan (18/08/1925 – 18/09/2007) ututangulie Mbele za haki kama ulivyotutangulia kuja duniani.

Nimajonzi sana kwetu hasa ukizingatia kuwa uliondoka katika tarehe ambayo kitinda mimba wako Mroki Mroki 'Father Kidevu' alizaliwa na ni siku kumi tu baada ya kufunga  ndoa Mroki.

Unakumbukwa na wengi sana maana ulikuwa ni mhimili mkuu katika familia, kipekee ni  Mke wako Mary O Nathan  pamoja na watoto wako wote, wajukuu wako na vitukuu.


Wananchi na majirani zako wa pale Kijiji cha Kinyenze,Kata na Tarafa
ya Mlali , Wilayani Mvomero mkoani Morogoro pia wanakukumbuka sana na kukuombea kila lililo jema katika mapumziko yako. 

Tunakumbuka maneno yako ya Mwisho uliotuachia watoto wako kuwa TUPENDANE, TUSAIDIANE na TUSHIRIKIANE, baba hakika hili linatendeka na tupo na  umoja uliotujengea na tunajivunia hilo daima.

Tunazidi kukuombea Baraka na pumziko jema maana sote uliotuacha tutakufuata kama tulivyo kufuata hapa duniani.

Jina la Bwana Lihimidiwe Amina.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages