Jukwaa La Sanaa la BASATA wiki hii lilipata wazungumzaji wa aina yake na kulifanya kuwa jukwaa lililochangamka na kuwa na mazungumzo ya zaidi ya masaa matano. Wasanii takriban 70 walikaa wakichambua maada mbalimbali
kuhusu mustakhabari wa sanaa katika nchi yetu. Jambo ambalo liliingiza
changamoto katika jukwaa hili, ni kuweko katika meza kuu wasanii wawili ambao walianza sanaa nchini na hatimae kuhamia ughaibuni ambako ndiko wanaishi kwa sasa.
Wasanii Salma Moshi aliyekuwa akijulikana kama Salma Nyoka, msanii wa kwanza wa kike kuchezea nyoka katika jukwaa, na ambaye alikuwa kiongozi wa vikundi vilivyotamba kama DDC Kibisa Cultural Troupe Super Mama Cultural Troupe na Ujamaa Cultural Troupe, na Abbu Omar, mwanamuziki aliyewahi kupigia bendi kama Urafiki na UDA Jazz ambae kwanza alihamia Kenya na kupiga na kurekodi na makundi kama Simba wa Nyika na Les Wanyika na pia kurekodi album kadhaa akiwa na kundi lake ambaye hatimae alihamia Japan ambako amekuwa akiishi kwa kupiga muziki na akiwa na waTanzania wengine kama Lista na Fresh Jumbe.
Mazungumzo yaligusia nyanja mbalimbali ikiwemo umuhimu wa kuwa na mikataba kabla ya kazi, kuboresha kazi ili kuweza kuuza nje, namna ya kujitambulisha duniani kwa kuwa na websites na blogs, na pia serikali kubadilika na kuweko mfumo wa uongozi wa sanaa kuanzia ngazi ya wilaya hadi Taifa. Katika mkutano huo, John Kitime Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanamuziki aliongelea fursa ya Bima ya Afya kwa wasanii, ambapo Salma Moshi alijitolea kuwalipia nusu ya ada wasanii wanne, na kumlipia bima kamili Mzee Kassim Mapili ambaye kwa sasa anasumbuliwa na moyo na figo. Abbu Omar pia aliamua kulipia Bima yake na kueleza kuwa katika nchi ya Japan ni lazima kila mwananchi kuwa na Bima ya Afya, kwani ugonjwa hauji kwa taarifa na matibabu ni gharama kubwa.
Mkutano huo ulianza saa tano na kulazimishwa kusimamishwa saa kumi, kwani wasanii bado walikuwa na mengi ya kuwauliza wasanii hawa nguli walioweza kuendeleza maisha ughaibuni kupitia sanaa
|
Baadhi ya wasanii wakimsikiliza Salma Moshi |
|
Mwandishi maarufu Khadija Khalili (mwenye daftari) akifuatilia maada |
|
Mwenyekiti wa CHAMRUMBA akiwa na Mzee Mapili |
|
Francis Kaswahili mwenye kofia Mwenyekiti TAFOMUDEA |
|
Abbu Omari mwanamuziki aishiye Japan |
|
Salma Moshi na Mzee Mapili |
|
Meza Kuu |
|
Group Picture |
|
Salma akiwa na baadhi ya wasanii aliowalipia sehemu ya Bima ya Afya
IMETAYARISHWA NA www.johnkitime.co.tz |
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)