Mgombea mwenza wa kiti cha urais, Bi. Samia Suluhu akisalimiana na baadhi ya viongozi alipowasili Jimbo la Ukonga kufanya mkutano wa kampeni eneo la Kipawa jijini Dar es Salaam.
MGOMBEA Ubunge Jimbo la Ilala, Mussa Hassan Zungu amemweleza mgombea mwenza nafasi ya urais Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu kuwa jimbo hilo limetenga kiasi cha shilingi milioni 300 kwa ajili ya kuwakopesha wajasiliamali wanawake na vijana kupitia vikundi vyao.
Zungu aliyasema hayo alipokuwa akitoa taarifa ya utekelezaji Ilani ya CCM kwa mgombea mwenza katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya Amana katika jimbo hilo jana jijini Dar es Salaam. Zungu alisema utekelezaji wa ilani ya CCM imefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 95 hivyo wananchi hawana budi kukipa ridhaa tena chama hicho kiendelee kufanya vizuri.
Alisema upande wa elimu jimbo hilo lilikuwa na shule sita za sekondari lakini katika utekelezaji wa ilani limefanikiwa kuongeza hadi kufikia shule 145 za sekondari huku wakifanikiwa kuboresha huduma za afya ikiwa ni pamoja na kupunguza gharama za X-Ray hospitali ya Amana, ambapo awali ilikuwa juu.
Akizungumza katika mkutano huo Bi. Samia Suluhu alisema kiasi cha shs milioni 300 kilichotengwa kwa ajili ya wajasiliamali na Jimbo la Ilala hakitoshi kutokana na wingi wa wajasiliamali hivyo kuahidi kuangalia njia ya kuwaongeza ili kitosheleze.
Alisema ilani ya CCM imepanga kurasimisha biashara za wajasiliamali ili waweze kuwa na vikundi vinavyotambulika pamoja na biashara zao kuwawezesha kunufaika zaidi. Alisema serikali ya CCM itaunda mamlaka maalumu ambayo itafanya kazi ya kusimamia biashara za wajasiliamali ili ziweze kupata masoko ya uhakika kwa bidhaa zao.
Aidha alisema wamepanga kuyaboresha masoko ya Kisutu, Kariakoo na Mchikichini ili yaweze kuwa na nafasi zaidi ya wafanyabiashara pamoja na kuyaboresha kiulinzi, usafi na usalama kwa wanaoyatumia. Alisema wanategemea kutengeneza nafasi mpya 3,150 za wajasiliamali katika masoko hayo ili kutoa fursa kwa wengine kunufaika na biashara hizo.
Alisema tayari maeneo mapya pia yametengwa ili kujenga masoko mapya kwa ajili ya wajasiliamali. Bi. Samia Suluhu alisema Serikali itaboresha madawati ya bodaboda na bajaji ili waweze kufanya kazi kwa kutambulika na kuongeza mipaka ya wao kuingia mjini ili kuondoa mvutano uliopo kwa sasa. Baadhi ya wanaCCM na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu (hayupo pichani) mkutano wa kampeni Jimbo la Ukonga kwenye Kata ya Kipawa jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu (hayupo pichani) katika mkutano wa kampeni Jimbo la Ilala Viwanja vya Amana jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu (hayupo pichani) katika mkutano wa kampeni Jimbo la Ilala Viwanja vya Amana jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu (hayupo pichani) katika mkutano wa kampeni Jimbo la Ilala Viwanja vya Amana jijini Dar es Salaam. Mgombea mwenza wa kiti cha urais, Bi. Samia Suluhu akifurahia mapokezi mara baada ya kuwasili katika mkutano wa kampeni Jimbo la Ilala Viwanja vya Amana jijini Dar es Salaam. Mgombea mwenza wa kiti cha urais, Bi. Samia Suluhu (kushoto) akizungumza jambo na baadhi ya viongozi wa CCM waliopo meza kuu mara baada ya kuwasili katika mkutano wa kampeni Jimbo la Ilala Viwanja vya Amana jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida. Mmoja wa makada wa CCM na Kiongozi wa Wamachinga na watu wenye ulemavu akielezea namna Serikali ya CCM ilivyowasaidia wafanyabiashara hayo jijini Dar es Salaam ikiwemo kuwajengea jengo la wamachinga 'Machinga Complex' Mgombea mwenza wa kiti cha urais, Bi. Samia Suluhu akisalimiana na baadhi ya viongozi waliohudhuria mkutano wa kampeni Jimbo la Ilala kwenye Viwanja vya Amana jijini Dar es Salaam.
[caption id="attachment_61565" align="aligncenter" width="760"] Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba 'Gadafi' (kushoto) akimbadika mgongoni mmoja wa wanaCCM picha ya mgombea urais wa CCM kwenye viwanja wa Amana jijini Dar es Salaam. Aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Nkenge, Asumta Mshama akizungumza na baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu (hayupo pichani) Jimbo la Ilala Viwanja vya Amana jijini Dar es Salaam. Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo la Ilala, Mussa Hassan Zungu akizungumza katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais, Bi. Samia Suluhu katika viwanja vya Amana jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Ramadhan Madabida akizungumza na baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu (hayupo pichani) Jimbo la Ilala Viwanja vya Amana jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wagombea wa nafasi za udiwani Jimbo la Ilala wakijitambulisha kwa wananchi katika mkutano wa hadharamadiwa. Baadhi ya waimbaji wa Band ya Mashujaa wakiwaburudisha wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika jimnboni Ukonga eneo la Kipawa. Mmoja wa wagombea nafasi za udiwani Jimbo la Ilala, Saady Khimji akiomba kura kwa wananchi katika mkutano wa hadhara. Kikundi cha sanaa ya ngoma za asili wakitumbuiza kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu Jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam. Kikundi cha sanaa ya ngoma za asili wakitumbuiza kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu Jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Ramadhan Madabida (kushoto) akizungumza na Meya wa Ilala Jerry Slaa ambaye pia ni mgombea ubunge CCM Jimbo la Ukonga katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu (hayupo pichani) eneo la Kipawa jijini Dar es Salaam.Imeandaliwa na www.thehabari.com
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)